Mabingwa Afrika

Cletus Cholla Chama!

Sambaza....

Kiungo mshambuliaji wa Zâmbia katika klabu ya Simba sc Cletus Cholla Chama aliendeleza moto wake katika mashindano ya Klabu Bingwa Africa Jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Simba jana ilikua dimbani kuiwakilisha nchini katika michuano hiyo ya klabu bingwa Africa dhidi ya Mbabane Swallors ya Swatziland.

Katika mchezo huo Simba ilipata ushindi mnono wa mabao manne kwa moja hivyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga hatua inayofuata. Magoli ya Simba yalifungwa na John Bocco mabao mawili, Meddie Kagere na Cletus Chama.

Cletus Cholla Chama

Achana na mchezo maridhawa waliouonyesha  SimbaSc wa pasi nyingi na burudani kama ilivyo tamaduni yao, kuna huyu kiungo Mzambia Cletus Chama aliekua “akitakata” katika eneo lá kiungo.

Chama alianza mpira akicheza kama kiungo akitokea pembeni upande wa kulia  lakini jinsi mchezo ulivyokua unaendelea alibadili upande na kuonekana kila sehemu ya kiungo cha Simba akisaidiana na James Kotei na Jonas Mkude.

Takwimu zake katika mchezo


Pasi muhimu 6

Kutengeneza nafasi 3

Msaada wa goli 0

Kupoteza mipira 5

Kadi nyekundu/njano 0

Nafasi ya wazi alizokosa 1

Kufunga goli 1

MO Amnyooshea mikono

Mmiliki wa klabu ya SimbaSc Mo Dewj alikuepo uwanjani kuwashudia vijana wake wakiwanyanyasa Mbabane Swallors Taifa.

Wakati Chama anafunga goli lá nne na lá mwisho Mo Dewji akashindwa kuficha hisia zake na kuamua kusimama kupiga makofi na kumpungia mkono kuonyesha kukubaliana na ufundi wa hali ya juu alioutumia Chama kufunga goli lile.

 

Pasi Ya Dilunga (HD)

Baada ya kuingia uwanjani kwa Hassan Dilunga kuchukua nafasi ya John Bocco, Cholla Chama alienda kucheza kama mshambuliaji pacha na Meddie Kagere.

Hakuifanyia makosa pasi swaafi aliyopokea kutoka kwa Dilunga. Akiwa kwenye pembe ya eneo la 18 katikati ya mabeki wawili alionyesha utulivu wa hali ya juu na kuweza kuwahadaa na kupiga shuti kali lililomuacha kipa wa Mbabane akiwa chini asiwe na lá kufanya.

Huyu ndio Mzambia Cletus Cholla Chama  “Wa Kimataifa”


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.