Ligi Kuu

Dakika za nyongeza zilikuwa nyingi- JKT Tanzania

Sambaza kwa marafiki....


Kocha wa JKT Tanzania, Abdallah amedai kuwa kilichowaua ni dakika nyingi za nyongeza ziliongezwa kwenye mchezo wao dhidi ya Simba.

“Hata sisi tulishangaa, mwamuzi anaenda kuongeza dakika 7. Kuna wakati uliona mwamuzi na mwamuzi msaidizi wanapingana, unaweza kujiuliza labda mwamuzi alikuja na kitu chake”.

Alipoulizwa kuhusu wachezaji wake kujiangusha amedai kuwa wachezaji wake walikuwa hawajiangushi.

“Unaweza kuona wanajiangusha lakini kuna wakati walikuwa wanapata injuries. Kuna mchezaji wetu kaumia leo ila wewe unaweza kuona kama wanajiangusha”.

Kuhusu Game plan yao kocha huyo wa zamani wa Prisons amedai kuwa walipanga kucheza mashambulizi ya kushitukiza.

“Tuliingia na Game plan ya kucheza mashambulizi ya kushitukiza kwenye mechi ya leo na ninashukuru tulijaribu kuifanya”.

Kuhusu kadi nyekundu amekiri kuwa iliwaua.

“Ni ukweli usiopingika kuwa kadi nyekundu ya mchezaji wetu ilituumiza sana, ila nawapongeza wapinzani wangu Simba kwa ushindi”. Alidai kocha huyo.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.