Kombe la Dunia

Ni Diamond tena Russia

Sambaza....

Mwimba muziki nguli  kutoka Marekani Jason Joel Desrouleaux, maarufu kama Jason Derulo amechaguliwa kutunga wimbo maalum wa Kombe la Dunia litakalofanyika Russia mwaka huu.

Jason Derulo  maarufu kwa uimbaji, uandishi wa nyimbo na kucheza kutoka Marekani, anafuata nyayo za Shakira, Anastaca na Pitbul waliwahi kuimba nyimbo hizo kwenye makombe ya dunia yaliyopita.

Jason Derulo

Wimbo huo wa kombe la dunia mwaka wa mwaka 2018 Russia utajulikana kama  ”COLOURS”. Hivyo kwa hisia za jina la nyimbo kabla ya kuusikiliza unaonyesha kutaka kuileta Dunia pamoja na kuonyesha  jinsi mpira unaweza leta watu pamoja.

” Ni heshima kutengeneza wimbo utakasherehekewa na timu zote pamoja na mashabiki. ”Colours” unawakilisha  bendera mbalimbali na tamaduni za nchi dunia nzima.” Jason Derulo , kijana aliyezaliwa September 21, 1989 huko Miramar, Florida Marekani.

Image result for World Cup Russia

Pia wasanii mbalimbali maarufu kutoka Africa wamechaguliwa kutengeneza wimbo wa kipekee  kwa kiutamaduni wa Kiafrika kutoka nchi za South Africa, Tanzania, Kenya, Ethiopia, Mozambique na Uganda.

Kwa Tanzania itawakilishwa na Diamond Platinums kutoka kwenye kundi la Wasafi. Ikumbukwe pia msanii huyu alitumbuiza katika Fainali za Mataifa ya Africa nchini Gabon mwaka 2017.

 

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x