Wachezaji wa Taifa Stars
Kombe la Dunia

Hii Hapa Njia ya Tanzania Kufuzu Kombe la Dunia

Sambaza....

Wapwa, droo kwaajili ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2026 kwa ukanda wa Africa itafanyika huko Ivory Coast  July 12 mwaka huu.

Tanzania ni miongoni mwa timu zinazasuburia kufahamu wapinzani wake ili kuendelea kujaribu kufuzu kombe la Dunia kama ilivyo kwa miaka yote. Ili safari hiyo itimie Tanzania inapaswa kupitia vigingi hivi.

Katika mgawanyiko huo ili kupata timu tisa zitakazoshiriki michuano hiyo mikubwa duniani timu zimegawanywa katika makundi(pot) sita.

Wachezani wa Tanzania “Taifa Stars”

Timu zilizopo Pot 1: (Africa’s level 1)
Morocco, Senegal, Tunisia, Algeria, Egypt, Nigeria, Cameroon, Mali na Ivory Coast.

Timu katika Pot 2: (Africa’s level 2)
Burkina Faso, Ghana, South Africa, DR Congo  Guinea, Cape Verde, Zambia, Gabon na Equatorial Guinea 

Timu katika Pot 3: (Africa’s level 3)
Uganda, Mauritania, Benin, Kenya, Congo Madagascar, Guinea-Bissau, Namibia na Angola.

Timu katika Pot 4: (Africa’s level 4)
Mozambique, Gambia, Sierra Leone, Togo, Tanzania, Zimbabwe, Central Africa Republic, Malawi na Libya.

Katika Pot 5: (Africa’s level 5)
Niger, Comoros, Sudan, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Swaziland, Liberia na Botswana.

Timu katika Pot 6: (Africa’s level 6)
Chad , Lesotho, South Sudan, Mauritius, São Tomé and Principe, Djibouti, Seychelles, Eritrea na Somalia.

Kombe la Dunia

Droo itatengeneza makundi 9 yeny timu 6 ambayo itakuwa na timu toka kila Pot yakwanza mpaka ya sita. Vinara wa makundi yote 9 ndio watakaocheza kombe la Dunia.

Kutakuwa na “best loser” wanne toka nafasi ya pili wataokwenda kucheza mtoano na mataifa mengine kuwania nafasi ya tisa kwa Africa.

Ikumbukwe Tanzania haijawahi kufuzu michuano hiyo mikubwa duniani na si tu Tanzania bali pia ukanda huu na majirani zetu wa Afrika Mashariki hatujawahi kutoa mwakilishi katika fainali hizo.

Sambaza....