Ligi Kuu

Dilunga alizamisha jahazi la Njombe Mji

Sambaza....

Timu ya soka ya Njombe Mji italazimika kupata ushindi katika mchezo wao mwisho wa ligi ili kujihakikishia kusalia ligi kuu soka Tanzania Bara baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi uliopigwa leo mjini Njombe.

Njombe Mji ambao walicheza vizuri wakikosa nafasi nyingi za wazi katika mchezo huo ambao umefanyika katika uwanja wa Sabasaba, waliruhusu bao pekee katika dakika ya 81 kwa shuti kali la umbali wa takribani mita 22 la Hassan Dilunga lililomshinda kipa Rajabu Mbululu.

Katika dakika ya 60 Njombe Mji walifanikiwa kuutumbukiza mpira wavuni kupitia kwa Jimmy Mwaisondola lakini mwamuzi wa mchezo huo akalikataa kwa madai kuwa mfungaji aliunawa mpira kabla ya kuukwamisha mpira wavuni.

Njombe Mji ambao wanaalama 22 watahitaji ushindi wa  hali na mali katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya wachimba almas Mwadui FC au safari yao ya kushuka daraja inaweza kuwaishwa mapema kama Ndanda watashinda dhidi ya Mwadui katika mchezo ambao utafanyika Jumatano katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mjini Mtwara.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x