Blog

Etienne kuendelea na Taifa stars

Sambaza kwa marafiki....

Kaimu kocha mkuu wa timu ya Taifa Tanzania, Etienne Ndayiragije, ataendelea kuinoa timu hiyo hadi mechi ya mwisho. Huu ni kwa mujibu wa katibu mkuu wa shirikisho la kandanda nchini wakati akijibu maswali ya wadau wa kandanda kupitia akaunti ya TFF katika mtandao wa tweeter.

“Kocha wa Muda wa Taifa Stars ataendelea kuongoza Timu katika mechi zote za Taifa Stars mpaka tutapomaliza kucheza na Sudan hatua ya mwisho ya CHAN.” Wilfred Kidao, baada ya kuulizwa swali na Hashim Mbaga kuhusu hatma ya kocha huyo ndani ya kikosi hicho.

Taifa stars ilisomga hatua inayofuata baada ya kuitoa timu ya taifa ya Kenya kwa mikwaju ya penati wiki iliyopita.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.