EPL

Gubu linavyowatafuna WAPINZANI wa Liverpool

Sambaza....

Sauti ya Shabiki wa Kandanda ni sehemu ambayo hukusanya maoni ya mashabiki kutoka katika mitandao ya kijamii. Haya ni maoni ya shabiki.


“Ndani ya misimu minne nitashinda taji moja”!! Ndivyo Jurgen Klop alivyowaambia waandishi wa habari misimu mitatu na nusu

Jamier Carragher alimuonya Klopp kuwa sio rahisi kihivyo na kosa kubwa sana kuahidi taji ndani ya misimu minne!! Alianza na Mfumo wake wa gegen pressing kwa wachezaji plastic Kama Sturidge alishindwa kabisa,wazito Kama Benteke walikoma!! Maumivu ya misuli yalishamiri ndani ya kikosi na madaktari wa viungo walimponda sana Klopp na hata Sir Alex Ferguson alidiriki kusema hajawahi kuona timu ina press muda wote?!! Klopp alijibu kirahisi tu kuwa anahitaji msimu mmoja kuweka misingi ya utimamu wa mwili kwa wachezaji wake.

kusajili kwa bei kubwa bali alianza kuingiza FALSAFA yake polepole kwa wachezaji aliowakuta huku akiwauza wale wote walioshindwa na kuingiza wapya polepole ndani ya timu!! Hadi Sasa ni wachezaji wanne tu wa kikosi cha kwanza aliowakuta wamebaki ndani ya kikosi na hata hivyo wengine hawana uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza!! Adam Lallana, Jordan Henderson,Firmino na Origi ndy pekee wamebaki kwenye kikosi cha Klopp!! Ninapoandika huu ni msimu wa tatu na nusu Klopp ametwaa mataji makubwa matatu UCL,FIFA CLUB WORLD CUP na UEFA SUPER CUP amezidi matarajio ya mashabiki wa Liverpool na sasa anaongoza ligi kwa tofauti ya point 16 huku akiwa na mechi moja ya kiporo dhidi ya Westham!!! Huyu ndy Klopp aliyetaka kuwageuza wasio na Imani wawe na Imani na timuWakati sherehe za mashabiki wa Liverpool zikishamiri sisi WAPINZANI wao tumebaki na gubu mioyoni mwetu huku tukisingizia VAR inawabeba Liverpool!! Tunasahau kuwa Klopp kambadili TAA kuwa KDB, Robertson kuwa MARCELO, Henderson kuwa MAKELELE n.k

Unathubutu vipi kusema Liverpool inabebwa kwa VAR wakati ina MANE,SALAH na FIRMINO walio kwenye fomu ya hatari sana kwa Sasa?? Hatuwaoni GINI na HENDO wanavyokaba?? Hatumuoni ORIGI alivyo super sub?!?
Tuacheni uchawi tuendelee kufuatilia soka Safi kutoka kwa vijana wa Klopp japokuwa inauma mno hasa mm Mr Mtawa ninaeichukia mnoo Liverpool lakini sina jinsi.

 

Mashabiki pinzani tujilaumu wenyewe kwa timu zetu kufanya maamuzi ya hovyo,eti leo Ancellot yuko Everton wakati United wanamkumbatia mpuuzi mmoja aitwae Sosha?,eti Massimiliano hana timu wengine wanampa Arteta timu!!?, Mourinho yupo Spurs halafu MLIPUKO FC wanafanya shangwe kumpokea lampard?? huu ni UHUNI ambao hata MASAU BWIRE hawezi kuufanya??.Namalizia kwa kusema hongera mjerumani JURGEN NORBERT KLOPP japokuwa roho inaniuma sana

MR MTAWA CHIEF EXECUTIVE OFFICER TABATA KIMANG


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.