Ligi Kuu

Haiwezekani Simba kutangazia ubingwa Namfua.

Sambaza....

Leo kutakuwa na mchezo kati ya Singida United na Simba ambao utachezwa katika uwanja wa Namfua mjini Singida.

Mechi hii itakuwa na kumbukumbu moja ambayo inaelekea kufanana . Msimu uliopita Simba wakiwa safarini kuelekea Singida , Yanga alikuwa anacheza na Tanzania Prisons.

Simba walikuwa wanaenda Singida kwa ajili ya kutafuta alama tatu ambazo zingewasaida kuchukua ubingwa, lakini Tanzania Prisons waliifunga Yanga na Simba kuwa mabingwa wakiwa njiani kuelekea Singida.

Leo hii Simba inahitaji alama moja tu kutangaza ubingwa wakiwa kwenye ardhi ambayo msimu jana walitakiwa kutangaza ubingwa wakiwa kwenye ardhi hii.

Mkurugenzi mtendaji wa Singida United, Festo Sanga amedai kuwa hawataruhusu Simba kutangaza ubingwa katika uwanja wao.

“Simba watatusamehe, tunahitaji alama tatu ambazo zitatuweka katika mazingira mazuri ya kuendelea kubaki daraja msimu huu”.

” Hatutoruhusu Simba watangazie ubingwa wetu, atatangazia sehemu nyingine lakini siyo hapa kwetu. Hapa lazima atage mayai matatu”- alimalizia mkuregenzi mtendaji wa Singida United.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.