Samatta akifanya yake
EPL

Hatimaye Samatta kucheza EPL wiki ijayo!

Sambaza....

Baada ya tetesi nyingi hatimaye Mbwana Samatta amewaaga wachezaji wenzake wa KR Genk kwa ajili ya kujiunga na ligi pendwa duniani , ligi kuu ya England.

Hii ilikuwa ndoto ya Watanzania wengi kushuhudia Mtanzania akiwa anacheza kwenye ligi ambayo ni kubwa ligi ambayo inafuatiliwa kwa kiwango kikubwa.

Kwa mjibu wa mtandao wa BBC umebainisha kuwa Mbwana Samatta atajiunga na Aston Villa kwa dau la paundi milioni 10.

Mtandao huo umebainisha kuwa Mbwana Samatta hatocheza kwenye mechi ya jumamosi hii kwa sababu wanashughulikia kibali cha kufanya kazi nchini England.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.