Blog

‘India ilijiondoa kombe la Dunia sababu ya Viatu’

Sambaza....

Inaaminika kuwa timu ya Taifa ya India, ilijiondoa kucheza kombe la Dunia mwaka 1950 baada ya kuambiwa wanatakiwa wasicheze peku.

Stori hii inaonekana sio ya kweli, ingawa swala la kucheza bila viatu lilijitokeza katika michuano ya Olympiki mwaka 1958 ambapo wachezaji wengi wa timu ya Taifa ya India walicheza ‘peku peku’ (bila viatu), na wengine wakiwa wamevaa soksi tu. Haya yalikuwa mashindano yao makubwa ya kwanza baada ya kupata uhuru tu.

Timu ya Taifa ya India (Miaka ya 1948)

India ilijikuta ikiingia katika kombe la Dunia baada ya timu za Philippines, Indonesia na Burma kujitoa na hivyo kuipa nafasi India ya kwenda moja kwa moja nchini Brazili kwaajili ya michuano hiyo. Timu shiriki hupewa fedha kwaajili ya maandalizi, hivyo sababu ambayo wengi waliamini pia mbadala na hii ya kucheza peku peku ilikuwa ni timu kushindwa kujigharamia safari zake, ambayo haikuwa kweli.

Timu ya Taifa ya India (Miaka ya 1948)

Kwa mujibu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini humo, sababu kubwa waliyotoa ilikuwa ni ‘kutokubaliana na katika uchaguzi wa timu na maandalizi kuelekea michuano hiyo’. Hivyo basi, India wanaamini hizo sababu za ‘peku peku’ na kukosa nauli hazikuwa sababu ya timu yao kushindwa kwenda kucheza Kombe la Dunia nchini Brazili. Hadi sasa ni takribani miaka 68, India haijanusa Kombe la Dunia.

Uruguay, 1950

Kombe la dunia mwaka 1950, Uruguay ndio walikuwa mabingwa kwa kuitandika 2-1 Brazili ambao walikuwa wenyeji. Fainali hizo zilichezwa Maraccana.

-Chanzo, indiatimes-


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.