Yanic Bangala akimdhibiti Ranga Chivaviro katika mchezo wa Shirikisho Afrika
Uhamisho

Jinsi Straika wa Yanga Anavyoleta Utata wa Usajili Huko Sauzi

Sambaza....

Klabu ya Yanga ilikua katika mawindo ya mshambuliaji mpya ambae atakuja kuziba nafasi ya Mayele ama atakwenda kuungana na Mayele katika safu ya ushambuliaji ya Yanga msimu ujao.

Miongoni mwa nyota waliotajwa alikua ni Ranga Chivaviro aliyekua akiitumikia Marumo Gallants ya Afrika Kusini iliyotolewa nusu fainali na Yanga katika kombe la Shirikisho Afrika.

Nyota huyo tayari ameshatambulishwa na Kaizer Chiefs kama mchezaji wao mpya lakini kumeibuka sekeseke la usajili wa nyota huyo baada ya klabu ya Richard’s Bay kuibuka na kusema Ranga ni mali yao.

Ranga Chivairo

Baada ya kufanya vyema akiwa na Marumo ambao walimpa mkataba wa mwaka mmoja ukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mwingine vilabu kadhaa ndani na nje ya Afrika Kusini vikaonyesha kutaka huduma yake.

Akiwa amebakisha miezi sita Richars Bay walimpa mkataba Ranga ili awatumikie msimu ujao, lakini klabu yake iliamua kutumia kipengele cha kumuongezea mwaka mmoja na kuamua kumuuza kwa Kaizer Chiefa kwa ada ambayo haikutajwa.

Tayari klabu ya Richard’s Bay imesema Ranga ni mali yao licha ya kutambulishwa na Kaizer Chiefs na hivyo itawalizimu chama cha soka Afrika Kusini SAFA na uongozi wa PSL kuliamua jambo hili mezani.

Sambaza....