Blog

Kahata kutua Simba baada ya Afcon

Sambaza....

Baada ya habari kuenea kuwa Fransic Kahata kasajiliwa na Simba , Tovuti hii iliamua kufuatilia vyanzo mbalimbali vya habari nchini Kenya kuhusiana na hizi habari.

Fransic Kahata ambaye yuko na timu ya taifa ya Kenya inayojiandaa na michuano ya Afcon nchini Misri, jana alizungumza na waandishi wa habari nchini Kenya.

Kagere(kushoto, wakati akiwa Gor mahia) na Kahata (Kulia)

Akizungumza na waandishi wa habari nchini Kenya kabla hajasafiri na timu ya taifa kwenda kwenye kambi ya timu ya taifa ya Kenya nchini Ufaransa, Kahata amedai kuwa mpaka sasa hajafanya maamuzi.

“Mpaka sasa hivi sijafanya maamuzi, nasubiri baada ya michuano ya Afcon ndiyo nitajua ni wapi ambapo nitapokwenda”- alisema kiungo huyo fundi ambaye mkataba wake na Gormahia FC unaisha msimu huu hivo atakuwa huru na habari zinadai Simba wana nafasi kubwa ya kumchukua.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.