Ligi Kuu

Kauli ya Mwinyi Zahera baada ya kichapo kutoka kwa Stand United.

Sambaza kwa marafiki....

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amesema timu yake imekosa bahati kwenye mchezo wa leo wa ligi ambapo wamefungwa kwa bao 1-0 dhidi ya Stand United.

Zahera amesema Stand hawakucheza vizuri tofauti na timu nyingine walizocheza nazo kama Mwadui lakini walikuwa na bahati kuwazidi.

Sauti ya kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera.

Bao pekee la Stand United limefungwa na Jacob Massawe katika dakika ya 88, kwenye mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.