Kelvin John akipongezwa na wenzake
Blog

Kelvin John kurudi shuleni sasa.

Sambaza kwa marafiki....

Mchezaji wa Serengeti Boys (Tanzania U17), Kelvin John ameiambia Kandanda kuwa alishindwa kuendelea na masomo yake kwa sababu ya kucheza mpira.

Katika mahojiano yake na Kandanda, anasema wakati wa majukumu ya timu ya taifa yeye alikuwa anatakiwa kufanya mtihani wa kidato cha pili kwaajili ya kuingia cha tatu, hili lilishindikana.

Kwa sasa Kelvin yupo kidato cha pili, na alitakiwa awe kidato cha tatu ila mwaka jana hakupata matokeo ya kumpeleka kidato cha tatu. “Ila kwa sasa napigania kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha pili mwaka.” Kelvin John.

Baada ya kumaliza michuano ya AFCON, sasa ameamua kurudi shule tena ili apate matokeo ya kumuwezesha kwenda kidato cha tatu mwakani.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.