Nahodha wetu
Mataifa Afrika

Kibabe tumeshatinga!

Sambaza....

 1. Uganda Hawaamini, Wanasema Sisi Wanga
  Penati Ile Ya Nyoni, Alipiga Chila Tenga,
  Wachezaji Wa Zamani, Mizimu Ndo Ilifunga,
  Fainali AFUKONI, Kibabe Tumeshatinga!

 

 1. Kwa Mkapa Uwanjani, Kiukweli Palifunga,
  Tumeujaza Pomoni, Kumbe Hamasa Ni Kinga!,
  Nyomi Mpaka ‘Vyooni’, Mubashara Na Luninga!
  Fainali AFUKONI, Kibabe Tumeshatinga!

 

 1. Msuva Yule Simoni, Walishindwa Kumchunga,
  Bocco Naye Kwa Madini, Mapande Yake Majanga,
  Gadieli Majinuni, Jini Mtoto Wa Yanga!
  Fainali AFUKONI, Kibabe Tumeshatinga!

 

 1. Nikimuwaza Yondani, Nyoyo Zetu Kazikonga,
  Ukuta Wa Babiloni, Wote Hawakuboronga,
  Manula Naye Golini, Karuka Na Kujinyonga,
  Fainali AFUKONI, Kibabe Tumeshatinga!

 

 1. Kessy Mtata Hasani, Alipanda Kama Winga,
  Gadieli Kushotoni, , Bwa’mdogo Toka Tanga,
  Maneno Mbele Mbeleni,Uganda Tumewagonga!
  Fainali AFUKONI, Kibabe Tumeshatinga!

 

 1. Samata Pale Dimbani, Aliwachezesha Vanga!
  Wakashika Mikononi, Wakawa Kama Wajinga,
  Penati Waya ‘Kimyani’, Sindano Tukawadunga!,
  Fainali AFUKONI, Kibabe Tumeshatinga!

 

 1. Musa ‘Mshika Ugoni’, Faridi ‘Ngenge Nganganga!’
  Kawaweka Mfukoni, Dogo Kama Singasinga,
  M-Tenerife Muhuni, Kama ‘Wa Jadi Mkunga’
  Fainali AFUKONI, Kibabe Tumeshatinga!

 

 1. Mudathiri Hayawani, ‘Kati’ Ukawabananga,
  Muda Kwanini Lakini, Ukaziba Zote Anga?
  Ukabaji Wa Bayani, ‘Miksa Miksa Na Michenga!’
  Fainali AFUKONI, Kibabe Tumeshatinga!

 

 1. Morisi Sura Usoni, Ni Kama Fundi Mjenga,
  Kakomaa Kama Nini, Kawaonesha Kiranga!
  Mzee Yule Makini, Kawavesha Hadi Kanga!
  Fainali AFUKONI, Kibabe Tumeshatinga!

 

 1. Joni Boko ‘Faru Joni’, Kacheza Kama ‘Kinyonga’,
  Alisogea Pembeni, Kama Bakari Mchunga!
  Mara Majalo Kwa Ndani, Ka Kona Ya Sangasanga!
  Fainali AFUKONI, Kibabe Tumeshatinga!

 

 1. Mungu Sio Athumani, Kikapulizwa Kipyenga! Bei Nusu Mitaani, Masaa Sita ‘Kitonga!’,
  Mama Nakufa Kinywani!, Machozi Yakatulenga!
  Fainali AFUKONI, Kibabe Tumeshatinga!

 

 1. Mpira Sio Utani, Kuchagua Ni Kupanga,
  Hadi Sasa Siamini, Tanzania Tunaringa?!
  Sasa Twapaa Angani, Tupo Bize Kuyajenga,
  Fainali AFUKONI, Kibabe Tumeshatinga!

 

 1. Magu Wetu Namba Wani, Ni Nani Wa Kumpinga?
  Kawapa Mamilioni, Na Viwanja Vya Kujenga,
  Na Pita Tino Jamani, Hajataka Kumtenga,
  Fainali AFUKONI, Kibabe Tumeshatinga!

 

 1. Wa Anda Seventini, Nao Magu Kawalenga,
  Katoa Na Bilioni, Waache Kuungaunga,
  Tiefuefu Peponi, Ni Mwisho Kutangatanga,
  Fainali AFUKONI, Kibabe Tumeshatinga!

 

 1. Makonda Vita Vitani, Saluti Martial Mhenga!,
  Umetupa ‘Rubudani’, Usiku Mida Ya Wanga!,
  Vinywaji Bei Nusuni, Tumepoteza ‘Vilonga!
  Fainali AFUKONI, Kibabe Tumeshatinga!

 

 1. Jeibii Jukwaani, Na Switihati Sepenga,
  Waliongeza Thamani, Refa Hawakumzonga,
  Wema Kalia “Jomoni!”, Na Mikono Akapunga!
  Fainali AFUKONI, Kibabe Tumeshatinga!

 

KUTOKA: Mkini na Alpha WAHENGA WA TAMBAZA “0766841987 na 0655595900” MAKAO MAKUU YA NCHI IDODOMYA-TANZANIA

Uzalendo KWANZA, Mambo mengine BAADAE!

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.