Ligi Kuu

Kikosi cha Tigana Lukinja chang’ara Moshi

Sambaza....

Timu ya shule ya Dar-es-salaam School Independence (DIS) vyema katika mashindano ya shule za mtaala wa kiingereza (International school) yaliofanyika wikiendi ilitopita huko mkoani Kilimanjaro.

Mashindano haya yalikuwa yakishirikisha shule kadhaa toka Dar-es-salaam kama Aga khan DSM, Brebuanuer, Aga khan Mombasa, IST, Morogoro International School, Rafiki , Moshi International School zote zikiwa katika mtaala wa Kimataifa nchini Tanzania.

Wachezaji na Walimu wa DIS wakiwa na makombe pamoja na medali zao

DIS iliibuka washindi katika kaundi la Timu za Soka za Wavulana chini ya Miaka 11 na Wasichana chini ya Miaka 9. Ambapo walishika nafasi ya pili kwa Wavulana wenye umri wa chini ya miaka 11 na kushika nafasi ya kwanza kwa Wasichana wa chini ya miaka 9 .

Timu hiyo pia kwa Wasichana chini ya miaka 11 walishika nafasi ya pili huku wavulana chini ya miaka 9 wakishika nao nafasi ya pili na kuihakikishia DIS vikombe 4 vya ubingwa.  Vikombe viwili katika nafasi ya kwanza na vikombe wiwili pia vya nafasi ya pili.

Timu hizi pia zinafundishwa na mdau wa Mtandao huu wa Kandanda.co.tz hii, Tigana Lukinja ambaye alikuwa akishirikiana na Ladislaus Ikingura, Amour Mgiriki, Miss Jane Msungu, Mr Songwe , Hallelujah na Diana.

Utaratibu huu wa kuwaendeleza vijana hivi kunaweza kutengeneza wachezaji wazuri walioandaliwa kisayansi kucheza katika soka la kulipwa.

Tigana (Katikati) akiwa na vijana wakati wa Kliniki ya Bundesliga huko Ghana.

Ticha Tigana ni kocha mwenye leseni ya ukocha ya CAF, ambaye pia amewahi kuchezea vilabu kadhaa wa kadhaa katika Ligi Kuu Tanzania bara, anaamini sana katika soka la vijana. Hivi karibuni alishiriki pia katika kliniki ya kuibua Vipaji ya Bundesliga iliyofanyika nchini Ghana.


Sambaza....