Blog

Kipa wa zamani wa Simba afariki dunia!

Sambaza....

Mlinda mlango wa timu ya soka ya Transit Camp Ahmad Waziri amefariki dunia leo asubuhi akiwa mazoezini baada ya kuanguka gafla.

Chanzo cha habari kinasema Ahmad Waziri alikua mzima kabisa kabla ya kuanza mazoezi ya kukimbia “Road Work” na wachezaji wenzake. Kipa huyo wa zamani wa Simba alifanya mazoezi ya kukimbia na timu kabla ya kuanguka gafla na kupoteza maisha.

Ahmad Waziri alikua anaitumikia timu inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ya Transit Camp inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza. Ambapo alikuwepo timu hiyo kwa mkopo akitokea JKT Tanzania iliyopo Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ahmad Waziri amewahi kuvitumikia vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu na madaraja ya chini kwa nyakati tofauti vikiwepo Simba sc, Majimaji fc, Mlale JKT na Spurrows fc “Discpline”

Pumzika kwa Amani Ahmad Waziri!


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.