Uhamisho

Kipa Yanga atimkia Kenya.

Sambaza....

Mlinda mlango wa zamani wa Timu ya Taifa ya Kenya “Harambee Stars” hatimae amepata timu mpya baada ya kukaa akiwa mchezaji huru tangu Disemba mwaka jana alipoachana na Mtibwa Sugar.

Farouk Shikalo aliyevunjiwa mkataba wake kwa makubaliano maalumu na Mtibwa Sugar  sasa anarudi nyumbani kwao Kenya na taarifa inasema atajiunga na Kakamega HomeBoys.

 

“Farouk Shikhalo atajiunga na Kakamega Homeboyz baada ya uhamisho wa Police FC kukosa kutekelezwa. Bado kuna maelezo machache ya kukamilisha, lakini kuna uwezekano atasaini mkataba wa miaka miwili na nusu. Homeboyz itatoa tangazo rasmi juu ya usajili mpya katika siku chache zijazo,” taarifa kutoka Kenya ilisema.

Shikalo aliyekuja nchini kwa mara ya kwanza  akiletwa na Wananchi Yanga na baada ya mkataba wake kumalizika alijiunga na KMC kabla ya msimu huu kuibukia Mtibwa Sugar ambayo hakudumu nayo sana kwani hata nusu msimu hakumaliza.

Kipa huyo mwenye uzoeufu mkubwa alioupata akiitumikia Bandari ya Kenya lakini pia amepita katika timu za vijana za Taifa za Kenya.

Sambaza....