Klop (Kocha wa Liverpool)
Blog

Klopp agoma kuvaa Suti kwenye mechi za Liverpool.

Sambaza....

Kocha wa Majogoo wa Jiji Liverpool, Jurgen Klopp  amekiri kuwa ni vigumu kwake kuvaa suti katika mechi za timu yake. Akielezea kuhusu kutoonekana kama makocha wengine, Klopp amesema kuwa ni vigumu sana kwa yeye kupumua vyema akiwa amevalia suti.

Klopp ameongeza kwa kusema kuwa, huvaa nguo inayomfanya ajisikie huru, awe na uwezo wa kuruka hapa na pale.

“ Nina suti nyingi za harusi, misibani kwahiyo hata mtu akiniambia nivae suti wala sio kitu cha ajabu kwangu”

“huwa sipendi kufikiria cha kuvaa kabla ya mchezo, kwahiyo nafurahi klabu inanipa vazi amablo naweza vaa na kufanya kila kitu uwanjani lakini sio suti” aliongezea Klopp.

during the Premier League match between Chelsea and Liverpool at Stamford Bridge on September 16, 2016 in London, England.

Liverpool kwa sasa inaongoza ligi ikiwa na alama  15  baada ya leo kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya NewCastle United nyuma ya mahasimu wao Man City wenye alama 10 katika mechi 5 walizocheza.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.