Mabingwa Afrika

Kocha Msouth: Tunajua jinsi ya kushinda hizi mechi.

Sambaza....

Klabu y Al-Ahly ilipata sare ya 1-1 dhidi ya Raja Casablanca katika mchezo wa raundi ya pili wa robo fainali na kushinda kwa jumla ya 3-2. Wakati mechi yakwanza  iliisha kwa matokeo ya 2-1 huko Morocco.

Kocha  huyo wa zamani wa Mamelodi Sundowns anaamini kuwa timu yake ilikuwa bora zaidi katika michezo yote  miwili.

“Ulikuwa mchezo mgumu. Tulimheshimu sana Raja, na tulikuwa bora katika mechi zote mbili,” Mosimane alisema, kulingana na KingFut.

“Tulipoteza penalti huku Cairo na nyingine huko Casablanca, kwa hivyo hakuna swali juu ya uwezo wetu. Hadi dakika ya mwisho, tulikuwa bora na karibu kushinda ikiwa sio kwa nafasi ya Mohamed Sherif iliyopotea.” Aliongeza kocha huyo wa Al Ahly.

“Tunahitaji kuboresha ufungaji wetu, lakini tuna uhakika katika uwezo wetu wa kusonga mbele. Tumethibitisha leo kwamba tunajua jinsi ya kucheza mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.” Pitso Mosimane kocha wa Ahly

Sambaza....