Sambaza....

Klabu ya Simba inakwenda kuandika historia mpya katika michuano mipya ya African Football League ambayo ufunguzi wake utafanyika October 20 katika mchezo wa Simba dhidi ya Al Ahly.

Simba itaanza na Al Ahly katika michuano hiyo mipya ambayo inachezwa katika mtindo wa mtoano huku kocha mkuu wa Simba Robert Oliveira akijinasibu kufanya vyema.

Akizungumzia droo hiyo, meneja wa Simba Roberto Oliveira alikiambia chombo kimoja nchini Misri “Nina furaha kukutana na Al Ahly, kwa sababu Simba ni timu yenye nguvu inayofanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa,” alisema na kuongeza;

“Sisi ni miongoni mwa timu 10 bora barani Afrika, na kwa sasa tuko katika nafasi ya saba. Tuna timu imara, mchanganyiko wa uzoefu na vijana, na nimeridhika kabisa na utendaji na mkakati tunaocheza nao.”

Robert Oliveira.

Rovertinho kwake anaona hii ni mechi kubwa na ngumu lakini pia ni nafasi kwao kusonga mbele. Mshindi wa mchezo huu atakutana na Mamelody Sundowns ama Petro Luanda.

“Naona hii ni fursa nzuri kwetu kufanya vyema na kuonyesha ujuzi wetu. Mechi dhidi ya Al Ahly itakuwa derby kali na mchezo mkubwa, na tunayo nafasi ya kujituma zaidi.”

Clatous Chama akimnyanyasa mchezaji wa Al Ahly walipokutana katika dimba la Benjamin Mkapa.

“Niko tayari kucheza popote. Pili, nawaheshimu washindani wote, lakini kwangu mimi soka si la siku za nyuma wala zijazo, ni kuhusu sasa. Washindani wote wanapaswa kuiheshimu Simba kwa sababu ni moja ya timu bora Afrika. Tuna timu imara, na ninapenda kucheza kwenye mechi za derby. Itakuwa mechi kali ya derby, na ninawaheshimu washindani wote.”

Sambaza....