Mshabiki wa Tanzania wakishangilia
Mataifa Afrika

Kwa elfu 13 tu unaishuhudia Taifa Stars nchini Misri.

Sambaza....

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetangaza gharama za tiketi za kutazama mechi za Fainali ya Africa (AFCON) inayotarajia kuanza mwezi ujao nchini Misri.

CAF imetangaza gharama hizo kwa madaraja mbalimbali, ambpo kwenye michezo ya hatua ya makundi ambayo itahusisha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” tiketi za daraja la itakuwa ni USD 29 (Tsh 66,700),tiketi za daraja la pili ni USD 18 (Tsh 41,400) na tiketi za daraja la tatu ni USD 6 (13,800 Tsh).

Hatua hiyo Taifa Stars itacheza michezo mitatu ambapo itaanza dhidi ya Senegal ikifuatiwa na mchezo dhidi ya Kenya na kumalizia hatua hiyo kwa kucheza na Algeria

Kwenye hatua ya robo fainali gharama ya tiketi daraja kwanza ni USD 35 (80,500 Tsh) kwa daraja la pili ni  USD 24 (55,400 Tsh) na daraja la tatu USD 12 (27,200 Tsh), huku hatua ya nusu fainali daraja la kwanza ni  USD 59 (135,700 Tsh),daraja la pili ni USD 29 (66,711 Tsh) na daraja la tatu ni USD 18 (41,400 Tsh).

Wakati mchezo wa mshindi wa tatu itakua USD 35 (80,500 Tsh) kwa daraja la kwanza ,USD 24 (55,400) kwa daraja la pili na USD 12 (27,200) kwa daraja la tatu, na Mchezo wa fainali daraja la kwanza ni USD 106 (243,821 Tsh),daraja la pili ni USD 44 (Tsh 101,208) na daraja la tatu ni USD 24 (55,400 Tsh).

Na shirikisho la soka nchini (TFF) limesema kwamba kwa yeyote mwenye nia ya kununua tiketi hizo za AFCON awasiliane na shirikisho mapema kabla ya kufungwa kwa muda wa maombi.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.