Lamine
Ligi Kuu

Lamine Moro agomea mazoezi Yanga

Sambaza....

Bundi anaendelea kuwepo kwenye paa la Yanga , baada ya kocha msaidizi wa Yanga Charles Boniface Mkwasa kumwondoa David Molinga kwenye kikosi cha Yanga na David Molinga kudai kuwa Charles Boniface Mkwasa anamchukia hali ambayo ilionesha kutoelewana kati yao .

Baadaye kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael kumrudisha tena David Molinga kwenye kikosi cha Yanga na kusafiri naye kwa ndege kuelekea Shinyanga wakati wachezaji wengi walisafiri kwa bus. Inavyoonekana kuna mgawanyiko kwenye kikosi cha Yanga kwa sasa.

Lamine Morro akimthibiti Shomari Kapombe

Mgawanyiko ambao umesababisha jioni ya leo beki hiyo Lamine Moro leo kugomea kufanya mazoezi na klabu ya Yanga. Hii ni  baada ya kuchukizwa na Uongozi wa Klabu Yanga kwa kuwa na upendeleo kwa baadhi ya wachezaji ndani ya Yanga. Upendeleo ambao unaonekana kama mgawanyiko.

Kabla ya kuanza mazoezi Leo jioni wachezaji wa Yanga walimchagua Moro kuwasemea wachezaji kwa Uongozi. Ila Uongozi wa Yanga uliopo Shinyanga ukawaambia wataongea Baada ya mazoezi ndipo Beki huyo akazila na akaenda kukaa kwenye Bus.

Kapama akimiliki mpira huku Lamine Moro akihakikisha hapiti.

Pia Kocha Luc Aymael na mshambuliaji wa Klabu hiyo David Molinga Ndama Falcao Leo jioni ameungana na kikosi na kufanya mazoezi ya pamoja kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwenyeji Mwadui FC Majira ya Saa 10:00 jioni kwenye dimba la Kambarage.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.