Anuary Kilemile akipambana na Ismail Mhesa katika mchezo wa TPL kati ya JKT Tanzania na Mtibwa Sugar
Blog

Ligi Kuu na mfumo wake wa mtoano na kushuka daraja

Sambaza....

Mfumo wa sasa wa Playoff uliowekwa katika ligi ya TPL umezaa matunda mazuri sana baada ya mpaka sasa timu zimebakiza mechi moja hakuna timu inayojua inashuka au kucheza playoff katika timu 8 ukiacha African Lyon iliyoshuka direct tayari.
Mambo yakoje tuangalie:

MECHI ZA MAAMUZI MAGUMU
Katika mechi zote za kunusurika kucheza Playoff au kushuka macho yote yatakiwa katika mechi 3 tu zinazohusu timu 6 matokeo haya wanafanya wengine wawe safe.

1. JKT vs Stand
2. Mbao vs Kagera
3. Mwadui vs Ndanda
4. Ruvu vs Alliance

RUVU SHOOTING
Timu hii haina Chaguzi ingine zaidi ya kushinda tu matokeo mengine yanaipeleka katika Pipa kuu la kucheza Playoff au kushuka direct.

MWADUI
Timu hii haina jinsi ingine ila kushinda tu ili kuweka kuingia katika Playoff maana kwa matokeo yeyote yale hhachomokikatika eneo hilo hivyo Bora kushika ili kujinasua kushuka daraja direct tu ila Playoff ipo palepale.

JKT TANZANIA
Timu hii ikishinda tu imeokoka bila kuangalia matokeo mengine ila Aki draw atakuwa na point 45 hapo ambazo zinampa pia nguvu ya kuwa juu kwa uwiano wa magoli ila itategemea na matokeo mengine akifungwa ameingia direct kwenye lile pipa ambalo zitaamuliwa kwa wastani wa magoli nani akae nafasi ipi.

KAGERA SUGAR
Timu hii haina matokeo mengine mazuri zaidi ya kushinda tu matokeo ya draw au kufungwa yanamuweka katika Pipa la uchaguzi wa nafasi tu.

STAND UNITED
Timu hii ikishinda imeepuka direct ila ikitoa draw itabidi tuangalie matokeo ya mechi ingine KUEPUKA au kuingia katika Pipa ikifungwa nakuna kuuliza kitu.

MBAO
Timu hii pia ni kushinda tu ndio mazuri kwake matokeo mengine kwake yeyote yyanamuingizakatika Pipa la kucheza Playoff au kushuka direct.

KWA MTAZAMO
Kuna timu zipo chini mfano biashara, Prisons na Singida kwa point ila kwa mazingira zzotehizi zipo Safe kwa 70% kutokana na michezo yyaona wapinzani wao kutokuwa na presha yeyote.

MWISHO
Mfumo wametoa ppichahalisi iliyotazamiwa Hongera sana Bodi/TFF kwa kuweka hili.
Kwa matokeo yeyote Timu mbili za chini 19 na 20 zinashuka direct FDL na timu ya 17 inasubiriwa na Geita Gold huku timu ya 18 iinasubiriwana Pamba katika michezo ya Playoff ingine ili kupata washindi wanabaki/kupanda TPL na wanaofungwa wanakwenda/kurudi FDL.
Ni mfumo unatoa nafasi 2 za wazi na nafasi 2 zilizojificha hizi ni za kuweka mazingira ya fair Play kwa wenye uwezo wafaidi.

MNYONGE MNYONGENI ILA KWA HILI TFF HONGERENI

Na: Hashim Mbaga


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.