Blog

Like father, like son. Unamwachia nini mwanao?

Sambaza....

Hii inaweza kuwa ‘ Like father like Son’ bora zaidi katika maisha ya soka kuwahi kutokea Dunia.

Sababu kubwa ikiwa ni nafasi ( position) kama unavyojua Goalkeeping ni special talent tofauti kabisa na namba za ndani.

Huwa ni wanafamilia wa Schmeichel Baba Peter ,Yeye aliitumikia timu ya Taifa ya Denmark pamoja na vilabu vingine kadhaa wa kadhaa lakini United ndiyo iliyomtambulisha vyema ukiachilia mbali Euro 1992.

Ambapo alifanya vizuri sana katika Career yake akiwa United kwa zaidi ya miaka 10 akipata mafanikio lukiki ikiwemo usiku wa maajabu ya Camp Nou 1999.

Kasper pichani (akiwa amebebwa na Baba yake mwaka 1992) yeye kama ilivyo ada mtoto wa nyoka hafundishwi kung’ata naye ni kipa hodari sana ikichezea Nice ya Ufaransa.

Alicheza Leicester City na kufanikiwa kutwaa nao ubingwa msimu wa 2014/15
na pia timu ya Taifa lao Denmark yeye ndiyo top golie.

Mawazo yangu hapa ‘like father like son’ zipo nyingi sana na yawezekana hata kurithi position lakini inapokuja swala la kutwaa ubingwa wa Premier league ndiyo naiona shughuli pevu.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.