EPL

Mambo matano usiyoyajua kuhusu John Terry

Sambaza....

Baada ya kutumia miaka 23 akiwa uwanjani kama mchezaji wa mpira wa miguu , jana John Terry alitangaza rasmi kustaafu kucheza soka la ushindani.

Yafuatayo ni mambo matano ambayo unatakiwa kuyajua kuhusu John Terry.

1: Alikuja Chelsea akiwa na miaka 14 kama mchezaji wa academy akitokea katika timu ya Westham. Alidumu Chelsea kwa miaka 20,huku akiwa nahodha wa timu hiyo kwa kipindi kirefu. Baada ya hapo aliondoka na kwenda Aston Villa ambapo amedumu kwa miaka mitatu.


2: Aston Villa na Chelsea vinaweza vikawa vilabu ambavyo vina historia nzuri sana katika maisha ya soka ya John Terry. Kwanini nasema hivo?. Chelsea itabaki kama timu ambayo amecheza kwa muda mrefu na kwa mafanikio makubwa sana. Lakini Aston Villa inabaki katika kumbukumbu zake kwa namna mbili, moja mechi yake ya kwanza akiwa na jezi ya Chelsea alicheza dhidi Aston Villa katika kombe la ligi akitokea benchi mwaka 1998. Pili, ametangaza kustaafu soka la ushindani akiwa na klabu ya Aston Villa.


3: Ameshinda jumla ya vikombe 18 akiwa na Chelsea, vikiwemo vikombe vitano (5) vya ligi kuu ya England, vikombe vitano vya Chama ya soka cha England vitano, kombe la ligi vitano. Pamoja na makombe ya ligi ya mabingwa barani ulaya na kombe la Europa.


4: Kuna habari Thierry Henry na John Terry wataungana kuwa makocha wa Aston Villa. Huku John Terry akiwa kocha msaidizi wa Thierry Henry. Hawa ni wachezaji wawili ambao walicheza katika timu tofauti kwenye ligi kuu ya England. Thierry Henry akichezea Arsenal na John Terry akichezea Chelsea. John Terry aliwahi kukiri kuwa alikuwa anatumia muda mwingi kufikiria namna ya kumkaba Thierry Henry usiku mmoja kabla ya mechi kati ya Chelsea na Arsenal kwa sababu Thierry Henry alikuwa mmoja wa washambuliaji bora na hatari kukutana nao katika maisha ya John Terry.


5:Amefanikiwa kucheza michezo 717 kama mchezaji wa Chelsea na huku akiitumikia timu yake ya taifa ya England katika michezo 78.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x