Mataifa Afrika

Mambo sita yaliyoinyima alama Stars Kwa Mkapa!

Sambaza....

Kuna mambo sita niliyoyaona yaliyomkwamisha Kim Poulsen kupata angalau alama moja dhidi ya Algeria licha ya kucheza nyumbani Kwa Mkapa.

1 Level of accuracy kwa maana ya usahihi wa matendo hasa kwenye kupasiana kutoka kwa mchezaji moja kwenda kwa mwingine (blind passes) zilikuwa nyingi na madhara yake ikawa ni kupoteza umiliki wa mpira (possession) bila sababu ya msingi na waweza kusema sisi ndiyo tulikuwa tunawakabia na kuwarejeshea mpira.

2 Study a game kwa maana ya kusoma mchezo na mahitaji yake kwa siku husikia ikiwemo “strong” na “weakness part” ya wapinzani. Mfano moja ya eneo lililo bora kwa Algeria ni mlinda mlango wao Rais M’bolhi ambaye aling’ara sana katika Kombe la Dunia mwaka 2014, Taifa Stars walikuwa wanapiga mbali kila muda kana kwamba ni kipa mdhaifu.

Feisal Salum akijaribu kumiliki mpira katikati ya wachezaji wa Algeria.

3.Composerness ya wachezaji ndani haikuwa kubwa kulikuwa na papara na hofu kwa 70% ya wachezaji walioanza kwenye kikosi ukitoa wale ambao wanacheza. nje kama Novatus Dismas Mbwana Samatta na Simon Msuva.

4.Lack of Individual ability hakukuwa na mpango wa mchezaji nmojammoja zaidi ya mpango wa pamoja wa timu, timu ilicheza kwa maelekezo ya benchi la ufundi hasa kwenye njia ya kupita mpira waliamini sana kwenye kutumia krosi kuliko kulazimisha kupita katikati kwa wachezaji wenye uwezo wa kupiga vyenga ( penetration) jambo hili unaweza kuliona baada ya kurejea kipindi cha pili mipira yote ilikuwa inalazimishwa kupita kwa mawinga hasa kule kulia na pale ambapo hakukuwa na mafanikio bado waliendelea kulazimisha.

George Mpole akimiliki mpira mbele ya mlinzi wa Algeria.

5 Physical Battle, ushindani kwa kutumia miili au maumbo baina ya mchezaji na mchezaji, wachezaji wa Algeria kwa 90% wanamaumbo makubwa na nguvu za kutosha hivyo kwenye kugombea mipira walikuwa wanashinda wao.

6 . Aerial / Duels Ball zote zilikuwa mali ya wageni vimo (body morphology ) viliwasuport hapa walifanikiwa mipira mingi na kutulazimisha tubadili mbinu ya mchezo ambayo yawezekana hatukuwa tumeifanyia kazi tangu awali.

Sambaza....