Blog

Man U na Arsenal hawachekani!

Sambaza....

zLigi Kuu nchini Uingereza imeendelea leo huku mchuano mkali wa kuwania ubingwa na “Top four” ukishika kasi hatua za lala salama, huku wakubwa wakiangukia pua.

Katika mchezo mchezo wa mapema ulishuhudia Everton wakiigaragaza Man United ya Ole Guna bila huruma. Everton wakiwa Goodson Park wamefanikiwa kuifunga Manchester United goli nne kwa sifuri.
Magoli ya Everton yamefungwa na Richarlison 13′ , Sigurdsson 28′, Digne 56′ na Walcott dakika ya 64.

Theo Walcot akishangilia goli dhidi ya Man Utd

Upande wa pili Arsenal nao wamekiona chamoto mbele ya wabishi wa London Crystal Palace baada ya kunyooshwa jumla ya mabao matatu kwa mawili.
Crstal Palace walipata mabao yao kupitia kwa Benteke 17′, Zaha 61′ na McArthur dakika ya 69.
Magoli ya Arsenal yalifungwa na Mesuit Ozil na Aubameyang katika dakika ya 47 na 77.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Man U kubaki nafasi ya sita wakiwa na alama 64 huku Arsenal wakibaki nafasi ya nne na alama 66.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.