Haji Manara msemaji wa klabu ya Yanga
Blog

Manara: Tunataka kuujaza uwanja Jumamosi!

Sambaza....

Kuelekea mchezo mkubwa kabisa Afrika Mashariki na Kati baina ya Yanga na Simba msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara ameanza kutema cheche huku pia akiweka wazi mipango yao kuelekea mchezo huo.

Haji Manara pia amezungumzia tofauti ya alama baina yao na wapinzani wengine katika Ligi ya NBC.

“Tunajua tupo katika nafasi nzuri, tukiwa mbele kwa point 13 tukiwa na uwiano mzuri pia wa mabao ya kufunga na kufungwa.” Manara.

Hassan Dilunga (kushoto) akiwania mpira na Djuma Shaban

Msemaji huyo pia ameonyesha ni kwa kiasi gani wamedhamiria kuujaza uwanja huku akitangaza neema kwa mashabiki wa Yanga wataokata tiketi kwenda uwanjani.

“Tunakusudia katika mchezo wetu dhidi ya Simba tutakaokua wenyeji sisi ndio tuujaze uwanja. Tutakua na promosheni kubwa ya hii mechi ambapo mashabiki wetu watanufaika haswa.” Hajji Manara.

Mashabiki wa Klabu ya Yanga.

Pia tutakua na punguzo maalum za jezi za msimu uliopita, mashabiki watapata jezi hizo na tiketi ya mzungu kwa 15,000 tu.
Hii ndio special offer kwa Wanayanga kuelekea mchezo wetu dhidi ya Simba wa Jumamosi April 30.” Aliongeza Manara.

Yanga wanatarijiwa kuwa mwenyeji wa Simba katika mchezo wa NBC Premier League. Katika mchezo wa raundi ya kwanza timu hizo zilitoka suluhu.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.