Mataifa Afrika

Mane kuikosa Stars

Sambaza kwa marafiki....

Kocha wa Timu ya Taifa ya Senegal Aliou Cisse amethibitisha kwamba Sadio Mane ataikosa mechi ya kwanza ya kundi C dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania katika mashindano ya AFCON 2019 .

Mane ataikosa mechi hiyo kutokana na kupata kadi mbili za njano kwenye mechi za kufuzu za mashindano hayo ya mataifa ya Afrika

Mane

“Kukosekana kwake hakutakiwi kutusumbua. Ni kweli uwepo wa Sadio una faida kubwa sana lakini bila yeye bado tupo imara. CAF wameamua hivyo kwahiyo hatutopinga.”

Mane alipewa kadi ya Njano kwenye mechi dhidi ya Equatorial Guinea Novemba 17, 2018 na nyingine dhidi ya Madagascar machi 23, 2019, licha ya kwamba haikuthibitishwa kwenye takwimu za mechi na CAF. CAF wametafutwa kuthibitisha .

Mane atacheza mechi mbili zitakazobaki baina ya Algeria na ya mwisho dhidi ya Kenya.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.