Sambaza....

Kiungo wa Manchester United na Serbia Nemanja Matic ameamua kutoa ya moyoni kuhusu mchezaji mwenzake wa Manchester United Anthony Martial.
Kiungo huyo wa Serbia na kipenzi cha kocha Josse Mourinho amemtaja mshambuliaji huyo wa Ufaransa na Man Utd kama moja ya kipaji maridhawa katika klabu ya Manchester United.

Nemanja Matic ” nadhani hajui ni mchezaji mzuri kiasi gani, ana kila kitu ambacho mchezaji wa Manchester United anapaswa kua nacho.

“Kama ningekua na uwezo kama wake na mwepesi nikiwa na mpira kama alivyo, ningekua sitoa pasi kwa wengine , ningekua nafunga goli kila mchezo.”

Ikumbukwe Anthon Martial amekua hapati nafasi ya kucheza kila mara, lakini Sasa kocha Josse Mourinho amempa nafasi na kuonyesha kiwango cha hali ya juu ikiwepo mchezo dhidi ya Chelsea alioweka kimiani mabao mawili.

Na katika michezo mitatu ya mwisho amefunga mabao manne. Lakini pia mchezaji huyo mkataba wake unaelekea ukingoni huku klabu hiyo ikihaha kutaka kurefusha kandarasi yake.

Sambaza....