Sambaza....

Wapwa, moja ya usajili ya maana pale kwa Wananchi katika msimu huu ni Mcongo Max Mpia Nzengeli mchezaji anayekupa vitu vingi sana ndani ya uwanja katika mchezo.

Ufanyaji wake kazi ni mkubwa katika maeneo yote ya uwanja na kwa ufasaha katika majukumu waweza kusema ni mchezaji aliyekamilika yaani “complete package”.

 

Akiongeza uwezo wa kujiamini na kutambua kwamba jukumu la kufunga lipo kwa mchezaji yeyote uwanja atafanya vizuri sana zaidi ya alipo sasahivi pale kwa Wananchi.

Ataonekana pia kwenye eneo la mwisho kwenye kitu cha muhimu zaidi kwenye soka ambacho ni kutupia kambani, ni kitu ambacho anatakiwa akiongeze kwake.

Max Nzengeli akimiliki mpira mbele ya viungo wa Azam Fc.

Mara nyingi amekuwa muoga kujaribu kupiga golini akiamini jukumu lile si lake, Max yeye anajioni ni wakutengeneza tu kwa lugha nyingine aongeze kijiuchoyo fulani anapolikaribia goli la mpinzani.

Ila kwa uchezaji wake na uwezo wake wa ufanyaji kazi kila kocha angependa kuwa na mchezaji wa aina yake katika timu yake kiwanjani.

Sambaza....