Shirikisho Afrika

Mchambuzi Awaomba Msamaha Wananchi Baada ya Kutinga Fainali

Sambaza....

Mchezaji wa zamani wa Njombe Mji pamoja na Majimaji Tigana Lukinja amewaomba radhi mashabiki wa Yanga baada ya timu yao kutinga fainali kwa kuiondosha Marumo Gallants katika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Tigana Lukinja ambae kwasasa anahudumu kama mchambuzi katika vituo vya TV E na Efm redio alisema haioni Yanga ikifika katika fainali ya michuano hiyo kutokana na kikosi walichonacho.

Baada ya filimbi ya mwisho kupigwa na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao mawili kna kufuzu kwenda fainali kupitia ukurasa wake wa instagram Tigana alisema “Nichukue fursa hii kuwapongeza sana Yanga kwa kufuzu fainali ya kombe la Shirikisho Afrika. Nyakati zinabadilika ‘Wananchi’ wamebadilika sana sana wamekuwa bora hatari (yaani weka mbali na watoto).

Wananchi Yanga.

Nimefurahi “wameniprove wrong” na ndiyo dhamira yangu kuu ilivyokuwa nilijua maneno yangu yatawagusa na kuongeza ari ya kujituma zaidi kama Mtanzania nawish kuona timu zetu zinasogea mbele.

Si tu aliwapa hongera zaidi Yanga lakini pia Tigana alitumia ukurasa wake kuwaomba radhi mashabiki wa Yanga na kukubali mapambano yanaendelea.

“Nasisitiza tena na tena hongera Yanga hongereni sana benchi la ufundi, wachezaji, wadau wa soka na Serikali kiujumla kwa msaada mkubwa. Pia niwaombe radhi mashabiki walioipokea vibaya kauli yangu niwahaidi kuwa Mzalendo wa wazi wakati mwingine kama mlivyohitaji

Aluta Continue hadi ubingwa hawa ndiyo Young Africa Sport Club a.k.a Wananchi,” alimaliza Tigana.

Sambaza....