Ligi Kuu

Mdhamini mkuu wa ligi ijayo apatikana

Sambaza....

Msimu huu ligi kuu ya Tanzania bara imemalizika bila ya kuwa na mdhamini mkuu wa ligi kuu. Akizungumza na waandishi wa habari, mkurugenzi mtendaji wa bodi ya ligi Boniface Wambura, amedai kuwa msimu ujao ligi kuu itakuwa na mdhamini.

“Msimu ujao ligi kuu itakuwa na mdhamini pamoja na wadhamini wengine wengi wadogo wadogo ndani ya ligi”.

Lakini pia Boniface Wambura amezisihi vilabu vya ligi kuu kutafuta wadhamini wengine wa ndani ya vilabu.

” Tunavihasa vilabu pia vitafute wadhamini wengine ndani ya klabu ili kupunguza makali ya uendeshaji wa vilabu”-Alisema mkuregenzi huyo wa bodi ya ligi.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.