Blog

Messi: Mambo bado magumu!

Sambaza....

Nahodha wa Barcelona Lionel Messi amewaonya wachezaji wenzake kuacha kufikiria kuwa wameshamaliza kazi baada ya kuwafunga Majogoo Liverpool FC jana kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Messi amesema licha ya ushindi wa mabao 3-0 lakini hajatosha kabisa kuweka matumaini ya kwamba tayari wameshafudhu kwenye fainali ambayo inatazamiwa kupigwa kwenye uwanja wa Wanda Metropolitano uliopo jijini Madrid Juni Mosi mwaka huu.

“Ingekuwa nzuri zaidi tungeshinda 4-0 kuliko 3-0, lakini ni matokeo mazuri, sasa tunakiwa kuungana zaidi kuliko wakati wowote, wote kwa pamoja, timu na mashabiki, tulisema mapema kwamba msimu huu tutashinda pamoja,” Messi amesema.

Katika ushindi wa jana Messi alifunga mabao 2 pekee yake na kumfanya kufikisha mabao 600 aliyoyafunga katika maisha yake ya soka akiwa sambamba kabisa na Cristiano Ronaldo ambaye naye ana mabao 600.

Bao lingine katika mchezo huo limefungwa na Luis Suarez katika dakika ya 25 ya kipindi cha kwanza, ushindi ambao utawafanya Liverpool kushinda mabao 4-0 katika mchezo wa marudiano utakaofanyika Juma lijalo mjini Liverpool.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.