Djuma katika majukumu yake akiwa na Klabu ya Simba
Uhamisho

Meza ya uhamisho: Jumamosi hii

Sambaza....

Mkusanyiko wa Tetesi na Usajili uliokamilika kwa siku ya leo kwa Tanzania. Tunaendelea kuandika….


Umekamilika: Maka Edward>> Latvia

Imeripotiwa kuwa Maka Edward atawaaga mashabiki wa klabu ya Yanga leo, tayari kwaajili ya kuelekea nchini Latvia kucheza soka la kulipwa.

Umekamilika: Mwadini Ally>> Azam Fc

Golikipa wa Azam Fc, ameongeza mkataba wake wa kuendelea kuitumikia klabu ya Azam Fc. Akiwa Azam Fc anapambana namba na Abalora.

Tetesi: Etienne Ndaringine >> Azam Fc

Klabu ya KMC imeshathibitisha kuwa kocha wake wa msimu uliopita Etiene hatakuwa tena na klabu hiyo. Etiene ameisaisia timu hiyo kumaliza nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu 2018/19 na kupata nafasi ya kushiriki kombe la shirikisho Afrika.

Kibwagizo: Singida Utd inahitaji wachezaji

Imewahi kuwa na wachezaji wazuri na kuwa timu yenye ushindani mkubwa, imetangaza kuwa wachezaji ambao wanahitaji kusajiliwa na klabu hiyo kwenda kufanya majaribio.

Taarifa kutoka Singida Utd

Tetesi: Masoud Djuma >>KMC

Kocha msaidizi wa zamani wa klabu ya Simba Sc anaelekea katika klabu ya KMC kuchukua nafasi ya Etienne aliyeondoka. Masoud Djuma kwa sasa haba timu baada ya kufukuzwa katika klabu yake ya awali nchini Kwake.

Umekalika: Bigirimani Blaise >> Namungo Fc

Mshambuliaji tegemezi wa Alliance Fc, akiwa ameifungia klabu hiyo magoli 10 msimu uliopita, amejiunga na Namungo FC ambayo imepanda daraja msimu huu.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.