Ligi Kuu

Mikono Ya Kabwili Inapingana Na Hukumu Yetu Kwake

Sambaza....

Nilikuwa naangalia marudio ya mechi ya Saint Louis na Yanga iliyochezwa Usherisheri.

Katikati ya mechi nilibaki naangalia umbo la golikipa wa Yanga, Youthe Rostand. Umbo ambalo linamfaa golikipa yoyote kuwa nalo.

Kimo chake kizuri , kimo kinachompa sifa ya ziada kama golikipa. Kuwa na umbo zuri hakutoshi kukufanya kuwa golikipa bora.

Kuna vitu vingi vya ziada ambavyo unatakiwa upigane kuvipata kwa kufanya mazoezi ili uweze kuwa golikipa bora kwenye mpira wa miguu.

Inawezekana msimu jana alionesha kiwango kilichovutia akiwa Africa Lyon, lakini ni ukweli usiopingika kuwa msimu huu amekuwa na kiwango ambacho siyo kizuri ukilinganisha na ƙkiwango alichokionesha akiwa na African Lyon msimu jana.

Youthe Rostand anakosa mtu wa kushindana naye kwenye kusaka namba katika timu ya Yanga ndiyo maana hana uchungu wa kuona kila siku anatembea kurudi nyuma.

Amekuwa na madhaifu mengi sana kwenye baadhi ya michezo ambayo amefanikiwa kukaa langoni.

Kwake yeye hata mipira ya chini imekuwa tatizo ndiyo maana mechi dhidi ya Ihefu Fc alisababisha iwe ngumu kwa Yanga na kusubiri mpaka mikwaju ya penati kuwatoa Ihefu FC.

Image result for youth rostand images

Habib Kiyombo alijaribu kuwaonesha Yanga madhaifu ya Youthe Rostand pale CCM Kirumba, lakini benchi la Yanga halikushtuka likazidi kumwamini.

Kumwamini kwao kunatokana na sababu moja tu nayo ni uzoefu , ana uzoefu katika udakaji lakini mikono yake haijakua.

Mikono yake ina umri mdogo ukilinganisha na umri wake halisi ndiyo maana siyo mwepesi hata anapokuwa anaamua kudaka mipira ya juu.

Kuna wakati maamuzi yake huwa mazito, huchukua muda mrefu mpaka kufanya maamuzi kitu ambacho kinadhihirisha siyo mkomavu kwenye akili yake na mikono yake.

Kuwa na umri mkubwa haimanisha waweza kufanya maamuzi yaliyokomaa, kuna wakati mtu mzima hufanya maamuzi yasiyo na ukomavu na mtu mwenye umri mdogo akafanya maamuzi yaliyokomaa

Ndiyo maana pale Yanga kuna watu Ramadhani Kabwili mwenye umri mdogo na Youthe Rostand mwenye umri mkubwa lakini maamuzi yao yanatofautiana.

Image result for Ramadhani kabwili images

Pamoja na kwamba tunamhukumu Ramadhani Kabwili kama mchezaji asiye na uzoefu kutokana na umri wake lakini mikono yake inatupa majibu tofauti na hukumu yetu.

Mikono yake inaonesha ukomavu mkubwa ambao tunaukosa kwa Youthe Rostand.

Jicho lako likiwa linashuhudia namna Youthe Rostand anavyoadhibiwa kwa magoli ya mbali, hadithi huwa tofauti kwa Ramadhani Kabwili ambaye kwake yeye mipira ya mbali ndiyo mipira ya kuonesha umwamba wake.

Umwamba ambao huufanya hata kwenye maamuzi yenye uharaka wa kudaka mipira ya juu inayotokana na ƙkona pamoja na mipira ya krosi.

Kuna wakati timu huzidiwa, wachezaji wa ndani wanaweza wakawa wamekata tamaa lakini mtu pekee ambaye hastahili kukata tamaa ni golikipa, golikipa ndiye mtu pekee ambaye anaweza rudisha morali ya wachezaji wenzake au kushusha morali ya wachezaji wenzake.

Pamoja na umri wake wa miaka 18 Ramadhani Kabwili ameonekana kuwa kiongozi mbele ya wachezaji viongozi tena wakongwe kama kina Kelvin Yondani.

Amekuwa akiwapanga vizuri kipindi timu inaposhambulia au kipindi ambacho timu inaposhambuliwa, ni ngumu kuona timu ikifungwa kutokana na mabeki kutojipanga vizuri kama goli ambalo Majimaji walifunga kwenye mchezo wa FA katika hatua ya kumi na sita bora 2017/2018.

Ni kawaida kwa mchezaji kutoka nje ya mchezo kwa dakika kadhaa, lakini ni kwa namna gani anaweza kurudi kwa wepesi kwenye mchezo.

Kabwili anapotoka mchezoni uwahi kurudi haraka na kuendelea kuiweka akili yake ndani ya mchezo.

Ni mdogo kiumri lakini ana akili ya kuitunza na kuilea familia, Donnarruma kaanza kudaka akiwa na miaka 15 mpaka leo hii ni baba wa Ac Milan, ni wakati sahihi kwa Kabwili kupewa jukumu la kuitunza rasmi Yanga.

 

Image result for Ramadhani kabwili images

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x