Mashindano

Misri kuandaa AFCON 2019.

Sambaza....

Shirikisho la soka barani Afrika ‘CAF’ limeipa uwenyeji nchi ya Misri kuandaa michuano ya Mataifa Afrika kwa mwaka 2019.

CAF imeitangaza Misri kuchukua mahala pa Cameroon ambaye alipokonywa uwenyeji huo baada ya kugundulika kushindwa kufanya maandalizi, hasa baada ya nchi washiriki kuongezeka na kufikia 24.

Misri iliomba uwenyeji sambasamba na Afrika Kusini mara tu baada ya Cameroon kupokonywa lakini CAF wameona waipe uwenyeji Misri kuandaa michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Juni mwaka huu.

Misri imeandaa Mashindano hayo mara nne na kutwaa mara tatu, iliandaa mwaka 1959 na kutwaa ubingwa, mwaka 1974 ilishika nafasi ya tatu, wakati mwaka 1986 na 2006 pia ilifanikiwa kutwaa ubingwa.

Mpaka sasa jumla ya timu 14 zimekwishafuzu kushiriki michuano hiyo ya mwaka huu, Huku Tanzania wakiwa na nafasi ya kufuzu kama watashinda katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Uganda huku wakiombea matokeo ya sare ama ushindi kwa Cape Verde dhidi ya Lesotho.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x