Blog

Mke wangu aliolewa na mwanaume mwingine-HAJI MANARA

Sambaza....

Afisa habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kwa sasa hana mke kwa sababu  ameshaachana na aliyewahi kuwa mkewe na tayari mwanamke huyo ameshaolewa kutokana na presha kubwa kutoka kwa familia ya upande wa mke wake.

Pamoja na kuachana na mkewe , Haji Manara amesema kuwa ana mpango wa kuoa mke mwingine ambaye atakuwa mzuri huku suala la tabia akiliweka kando kidogo.

Moja ya mikutano ambavyo timu inaweza kutangaza viingilio au utaratibu wa mapato yao. Pichani ni Haji Manara, Msemaji wa Simba SC.

” Kulikuwa kuna presha kubwa sana upande wa mke wangu hadi nikafikia kuamua kuachana naye.Siku chache baadaye nikasikia ameolewa, wala sikushituka kwa kuwa hili nilijua lilikuwa limeandaliwa na linakwenda kuwa hivi.

“Kwa sasa nasubiri kwanza lakini nitaoa na mwanamke ninayetaka kumuoa lazima awe mrembo sana. Nataka mwanamke mrembo hasa, suala la tabia litafuatia.” Alimalizia kwa kusema hivo wakati anazungumza na Zamaradi TV


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.