Stori

Mo Dewji Anairudisha Simba Nyuma.

Sambaza....

Nimesoma andiko la MO (Mohamed Dewj) kuhusu masuala ya “Transformation” ndani ya Simba SC. Ni andiko lenye mistari miwili, lakini lina maana zaidi ya mistari hiyo. Baadae MO akaja kulifuta andiko lile linalofikirisha. Sijali!

Sijui kwanini aliandika na baada ya muda akafuta. Sijui. Kimsingi MO Dewji ana hoja. Shida ni muda aliochagua kuileta mezani hoja yake. Shida ni hii tu.

Nafahamu machungu ya mtoa pesa ili mambo yaende. Lakini MO hakupaswa kuja kipindi hiki ambacho Wanasimba wako pamoja kwa ajili ya kujenga timu imara ya msimu ujao.

Tweet ya Mo Dewji kabla ya kuifuta.

Vitu vingi ndani ya Msimbazi vimetulia kwa sasa na kila mmoja anatazama mabosi wanamsajili nani. Hiki hakikupaswa kuwa kipindi cha masuala ya Transformation ( Japo hazuiwi / hapangiwi muda wa kufanya / kuandika anachokiamini).

Post ya MO ni post iliyokwenda kuvirudisha vitu nyuma baadhi ya vkwa kiasi. Inavunja watu moyo.

 

Sambaza....