Blog

MOLINGA alitakiwa aondoke na MWINYI ZAHERA

Sambaza....

 

Habari ambazo zinaenea kwa Kasi muda huu ni kuhusu David Molinga kuachana na klabu ya Yanga kwa madai ya matatizo ya nidhamu ambayo amekuwa akiyaonesha mara kwa mara.

Kwangu Mimi nano “matatizo ya nidhamu ” linatumika kuuficha ukweli , ukweli ambao David Molinga ndiyo unamfanya aondolewe katika timu hiyo ya Kariakoo mjini Dar es Salaam.

David Molinga amekuwa siyo mchezaji ambaye ana kiwango kikubwa kama mchezaji wa kulipwa , anaonekana ni mchezaji wa kawaida tu katika kikosi hicho cha Yanga.

Hajawafurahisha wengi kama mchezaji wa kulipwa , kiwango chake hakina tafasri kuwa yeye ni mchezaji wa kulipwa ndiyo maana Yanga wanaona ni bora waachane naye na kuchagua njia nyingine.

Nishawahi kumsikiliza aliyewahi kuwa kocha wa Yanga , Mwinyi Zahera aliwahi kusema kuwa David Molinga ni mchezaji hatari na amemsajili akijua kabisa kuwa ni mchezaji hatari kutokana na yeye kumuona katika ligi ya nyumbani kwao Congo.

Tuanzie hapa , Mwinyi Zahera alikuwa anamuamini David Molinga, yeye ndiye aliyekuwa anaamini na alikuwa anajua wapi ubora wa David Molinga ulipokuwepo ndiyo maana hakusita kumpa nafasi kila uchwao.

Hata alipoondoka hakuna ambaye alibaki kumwamini David Molinga kuwa anaweza anafanya kitu kikubwa kwa sababu mtu ambaye alikuwa anamwamini tayari alikuwa hayupo , ilikuwa lazima tu Baada ya kuondoka Mwinyi Zahera , David Molinga alikuwa anafuata .

Sambaza....