Blog

Molinga na Luc Eymael waenda Shinyanga kumvaa Mkwasa

Sambaza....

Kwa mujibu wa David Molinga , Charles Boniface Mkwasa hampendi David Molinga . Kauli hii aliitoa David Molinga baada ya kuachwa kwenye kikosi cha Yanga kilichoenda Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga.

Baada ya Charles Boniface Mkwasa ambaye ni kocha msaidizi wa Yanga kutangaza kumwacha David Molinga kwenye kikosi cha Yanga , kocha mkuu wa Yanga ambaye alikuwa nje ya nchi alitangaza kumrudisha David Molinga kwenye kikosi cha Yanga.


Leo hii Luc Eymael ambaye ndiye kocha mkuu wa Yanga pamoja na David Molinga walionekana kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakienda Shinyanga kwa ajili ya mechi ya Mwadui FC.

Hii inaenda kuwakutanisha kwa mara ya kwanza David Molinga na Mocha msaidizi as Yanga , Charles Boniface Mkwasa ambao wanaonekana hawako sawa kwa asilimia kubwa , pia inaenda kuwakutanisha Luc Eymael aliyetengua maamuzi ya Charles Boniface Mkwasa.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.