Blog

Mpwa akiichambua Stars

Sambaza....

Wapwa: Niwapongeze sana timu yangu Taifa Stars kwa kututoa kimasomaso kwa ushindi mujarab ya 3-1 wachezaji wote walitoa mchango mkubwa tu unaopenda lakini niliiona nafasi ya Exposure na Experience ya wanaocheza nje kiufundi Zaidi

Allmost composer zao zilikuwa kubwa sana Captain Diego aliamua jana kurejea yule ya Mbagala Market (Africa Lyon) aliyekuwa anataka kwenda Simba kabla ya goli nilimwambia mtu moja kuwa Nahodha alikuwa na siku nzuri kwa kuwa kaamua kutoa alichonacho

Akitumia uzoefu wake kwenye goli alionesha utulivu mkubwa sana kwa kuchange miguu first touch na finishing yake kwa miguu mwingine alionesha ubora wa footwork yake binafsi sina hata chembe wala mashaka na ubora wake

Kusudio langu hapa ni kukuambia uwekezaji kwa vijana na kuwapa uzoefu ikiwemo exposure ya nje jaribu kutizama usahihi mkubwa wa matendo kwa vijana wanaocheza nje waliokuwepo kwenye mchezo wa jana

Mnielewe sina maana ya wanaocheza ndani walikosa sifa hizo hapana maana yangu inakuja kwenye technical quality basic movement nk ili hali ukiwatizama kiufundi kabla ya kupokea na kupeleka mpira.

Kifupi nachoweza kusema kuna faida ya kupush wachezaji wetu kwenda kucheza nje kwa maana ya kupata exposure ambayo ni factor muhimu sana kwenye soka

Sitaki kumtaja moja moja kwa jana na mchango wake ,lakini nadhani wenyewe
mlijione ,nadhani tukiwa na wachezaji wengi nje tunaweza kufanya vyema katika medani ya soka kwa jana tulianza na wachezaji 6 wanaocheza nje

Tupush wachezaji wetu watoke baada ya miaka 3-5 tunaweza kuwa na timu imara sana sisi tuna faida hasa kwa vijana hawa wenye umri kati 18-23

kundi la akina Dismas ,Mbappe Ben na wengineo na hata wale wasioitwa kama Omary Marungu na huyu Rajabu Ally Mbungu anayecheza kwa U-17 PSG


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.