Mataifa Afrika

Mshambuliaji mpya wa Simba, Chama waachwa timu ya Taifa.

Sambaza....

Kocha wa Timu ya Taifa ya Zambia Alijosa Asanovic ametaja kikosi cha wachezaji 25 kuelekea kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwakani dhidi ya Ivory Coast na Comoro itakayochezwa Juni 3 na 7 mtawalia.

Katika kikosi hicho hayupo mshambuliaji Mosses Phiri ambae inasemekana amemalizana na Simba akisubiri kujiunga nao msimu ujao kwani ameshaaga katika klabu yake ya Zanaco. 

Clatous Chama

Pia katika kikosi hicho Chama hajaitwa na kocha wa Chipolopolo Asanovic kutokana na majeruhi na nafasi yake imechukuliwa na Rally Bwalya wa Simba pia.

Kikosi kamili cha Chipolopolo kinaundwa na wachezaji, Toaster Nsabata (Sekhukhune), Charles Kalumba (Red Arrows) na Cyril Chibwe (Hana timu).

Kiungo wa Simba Rally Bwalya akiwatoka walinzi wa Azam Fc.

Mabeki ni Frankie Musonda (Raith Rovers-Scotland), Tandi Mwape (TP Mazembe-DR Congo), Miguel Chaiwa (Athletico), Dominic Chanda (Kabwe Warriors), Benedict Chepeshi (Red Arrows), na Shemmy Mayembe (Zesco United).

Eneo la kiungo kuna Roderick Kabwe (Sekhukhune-Afrika Kusini), Enock Mwepu (Brighton-England), Emmanuel Banda (Djurgardens-Sweden), Kings Kangwa (Arsenal Tula-Russia), Rally Bwalya (Simba -Tanzania), Prince Mumba (Kabwe Warriors), Lubambo Musonda (AC Horsens-Denmark), Kelvin Kampamba na Spencer Sautu, (Zesco United), Lameck Banda (Maccabi Petah Tikva-Israel) na Edward Chilufya (Midtjylland-Denmark).

Patson Daka

Wachezaji wa nafasi ya ushambuliaji walioitwa ni Fashion Sakala (Rangers-Scotland), Evans Kangwa (Arsenal Tula-Russia), Ricky Banda (Red Arrows), Gamphani Lungu (SuperSport United-Afrika Kusini) na Patson Daka (Leicester City-England.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.