Uhamisho

Mshambuliaji Simba atambulishwa timu yake mpya

Sambaza....

Mshambuliaji na nahodha wa zamani wa Simba Opa Clement aliyejiunga na timu yake mpya ya Besiktas ya wanawake tayari ametambulishwa na timu yake hiyo mpya akiwa tayari kuanza kuwatumikia Waturuki hao.

Opa aliyeiacha Simba ikiwa kileleni baada ya mzunguko wakwanza kumalizikia nayeye pia akiwa kinara wa mabao kwa kufunga mabao tisa katika michezo tisa aliyocheza mpaka Ligi ya Serengeri ya wanawake inasimama.

 

Kupitia tovuti ya klabu Besiktas imemtambulisha nyota huyo kutoka Simba huku akijiunga na wenzake moja kwa moja mazoezini baada ya kumaliza kupima afya.

“Usajili wetu mpya Opa Clement amefuzu vipimo vya afya vilivyofanyika katika hospitali ya Fulya,” taarifa hiyo ilisema

Opa Clement akiwa mazoezini na timu yake mpya Besiktas.

Tayari klabu yake ya Simba juzi ilishatoa taarifa rasmi yakumtakia kila lakheri nyota wao huyo aliyefanya vyema katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuwepo katika kikosi bora cha mashindano hayo iliyofanyika nchini Morocco.

“Karibu Besiktas Vodafone Opa Clement Tukumbuke. Timu yetu ya Wanawake ya Besiktas imefanikiwa kuingia mkataba na Opa Clement Tukumbuke, mshambuliaji huyo alikua akiitumikia Simba Queens,” taarifa hiyo iliongeza.

Sambaza....