Mataifa Afrika U17

Mwakyembe aitembelea Serengeti boys

Sambaza....

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, leo hii Jumamosi Januari 20, 2018 ameitembelea kambi ya timu ya taifa ya vijana walio chini ya wa miaka 17, Serengeti boys iliyopo kwenye hostel za shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF

Katika ziara hiyo Mwakyembe aliweza kuona jinsi vijana hao wanavyofanya mazoezi chini ya kocha Kim Polsen raia wa Denmark

Akizungumza na vijana hao waziri Mwakyembe, amewataka wajitume zaidi kwa ajili ya Tanzania pia aliwaachia ujumbe wa Serikali vijana hao

Dk Mwakyembe akiwapa salamu Serikali vijana hao amewaambia kuwa Serikali ina waamini, na wanalojukumu la kuhakikisha wanaipeperusha vema bendera ya Tanzania amewataka kupambana kwa ajili ya Tanzania na kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye kila michuano watakayoshiriki, pia alilitaka benchi la ufundi la kikosi hicho linaloongozwa na Kim Polsen kuhakikisha wanawapa mafunzo mazuri kwa ustawi wa vijana hao

Dk Mwakyembe amesema anaamini vijana hao wataimalika chini ya TFF inayoongozwa na Rais Wallace Karia “Naamini mtaimalika na kuwa bora kwa maana hata TFF na ina ari na morali kubwa” alisema Dk Mwakyembe

Katika ziara hiyo Dk Mwakyembe alipata nafasi ya kuitazama Serengeti boys ikicheza michezo miwili ya kirafiki, ambapo katika mchezo wa kwanza vijana hao walicheza dhidi ya kituo cha Bombom na kutoka sare ya kufungana bao 1-1 huku katika mchezo wa pili walishinda 4-1 dhidi ya Sekondari ya Makongo

Serengeti boys ipo kambini tangu januari 28, 2018 ikijiandaa na michuano ya Cecafa challenge cup U17

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x