Mataifa Afrika U17

Watanzania wanatakiwa kuwa wavumilivu- Ammy Ninje

Sambaza....

Mkurugenzi wa ufundi wa TFF, Ammy Ninje amewataka Watanzania wawe wavumilivu ili kufikia mafanikio kwenye timu zetu za taifa.

Akizungumza na mtandao huu wa kandanda.co.tz amedai kuwa lazima tuanze kujifunza kutokana na makosa yetu.

Kufikia maendeleo ya mpira wa miguu ni lazima kuwe na hatua za kufikia maendeleo ya mpira wa miguu, hivo tunatakiwa kuwekeza sana.

Ammy Ninje amedai kuwa tunatakiwa kuwekeza ili kupata vijana bora ambao wataisaidia timu yetu ya Taifa. Pia Ammy Ninje amedai kuwa kuna sehemu walikosea.

Sehemu ambayo ameisema kama eneo ambalo walikosea ni sehemu ya kupata wachezaji sahihi katika kikosi cha Serengeti boys.

Ametolea mfano kuwa eneo la golikipa hawakupata golikipa bora ambaye angeisaidia timu hii katika michuano mikubwa kama hii.

Hili ni eneo ambalo Ammy Ninje ameahidi kulifanyia Kazi. Watahakikisha kuwa wanawekeza kuangalia vipaji bora ili viwepo kwenye timu.

“Tulikosea kwenye namna sahihi ya kupata wachezaji ambao ni bora hasa hasa eneo la golikipa. Hivo tutawekeza ili kuwepo na njia nzuri ya kuwapata wachezaji bora.

” Watanzania tunatakiwa tuwe wavumilivu kwa sababu kufikia mafanikio ya mpira wa miguu inatakiwa kabisa kupitia hatua ambazo ni kubwa”. Alisema Mkurugenzi huyo wa ufundi wa TFF.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x