Inonga Baka "Varane"
Blog

Nani anashangaa Inonga kuitwa kikosini?

Sambaza....

Wapwa, Binafsi sishangai Henock Inonga kuitwa kwenye timu yake ya Taifa kwa kuwa amewahi kuitwa.

Ni ukweli usiopingika Taifa hilo lina changamoto ya uteuzi kuwakilisha nchi kwa kuwa hao si matajiri tu wa madini bali hata huku kwenye soka.

Taifa hilo lina maelfu ya wachezaji wanaocheza pande mbalimbali za Dunia kwenye ligi yenye ushindani na hata zile zisizo na ushindani.

Hii humpa fursa kubwa Kocha wao kuchagua Wachezaji wake ,nini maana yake hapa

Inonga anastahili kupongezwa kwa kujumuisha kwenye kikosi kwa Taifa lenye ushindani kama hilo

Pia huu ni ushindi kwa waliomchagua msimu uliopita kuwa mlinzi bora wa msimu kwa NBC ( Wana jicho)

Sambaza....