Blog

Nani Galacha wa Kandanda 2018?

Sambaza....

Moja ya dhumuni kuu la tovuti yetu ni kusheherekea mafanikio ya watu ambao wanafanya vizuri katika ulimwengu huu wa soka kwa Tanzania. Kwa mwaka 2018, (#GWK2018TZ) tumeaandaa vipengele vikuu vitano ambavyo vinaenda kuwatunuku watu 15 katika kandanda la Tanzania (Wachezaji wote wanaocheza Tanzania na Watanzania wa Nje), hawa tunawaita Magalacha wa Kandanda 2018 (Galacha wa Kandanda 2018).

Waandishi na Wachambuzi wa Kandanda kwa pamoja wameandaa orodha ya wachezaji hao ambao wasomaji wetu, makocha, manahodha na Wadau wengine watawapigia kura kupata galacha mmoja kila kundi. Tumekuwekea maelezo pia kwanini tumewachagua hawa kuwania tunzo zetu. Mwisho wa kupiga kura ni tarehe 16/01/2019


Ni nani anafaa kuwa mchezaji bora?

Emmanuel A. Okwi (Simba Sc)-Aliwahi kuishi Msimbazi, akawa kipenzi kikubwa cha mashabiki wa mtaa unaoitwa msimbazi. Alifanikiwa kujipenyeza kwenye kilindi cha mioyo ya mashabiki wa Simba. Alipoondoka waliumia sana, lakini mwaka 2017 alifanikiwa kurudi rasmi. Na msimu Jana aliganikiwa kuwa mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania bara akiwa na magoli 20 huku akiisaidia Simba kubeba ubingwa wa ligi kuu kwa Mara ya kwanza baada ya miaka 5. Msimu huu mpaka sasa amefanikiwa kufunga magoli 7 kwenye ligi kuu na ameisaidia Simba kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Heritier Makambo (Yanga SC)- Alijiunga na Dar Young Africans katikati ya mwaka 2018. Amekuwa msaada mkubwa na dira ya Mafanikio kwa klabu ya Yanga mpaka sasa akifunga mabao 11 kati ya mabao 35 ambayo yamefungwa na timu hiyo msimu 2018/19 ndani ya mwaka huu na kuisaidia kuwa kinara wa ligi ikifikisha alama 50 katika mechi 18 ambazo wamecheza mpaka mwisho wa mwaka 2018 kwa msimu 2018/19.

Jonas Mkude (Simba Sc) amefanikiwa kuipa ubingwa klabu yake ya Simba baada ya kuukosa kwa miaka 5, akicheza kama kiungo muhimu, Pia amesaidia kuipeleka Simba katika hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika huku akicheza katika michezo yote minne ya awali na akifanikiwa kufunga bao moja kati ya magoli 12 waliyoyafunga simba katika michuano hiyo.


Kocha wa Mwaka

  • Patrick Aussems (Simba Sc*) (67%, 6 Votes)
  • Mwinyi Zahera (Yanga Sc*) (22%, 2 Votes)
  • Selemani Moja (Lipuli Fc*) (11%, 1 Votes)
  • Ettiene Ndayiragije (KMC Fc*) (0%, 0 Votes)

Jumla ya Kura: 9

Loading ... Loading ...

Nani bora zaidi kwa wachezaji wanaocheza soka la kulipwa?

Abdi Banda ( Baroka FC, Afrika Kusini)-Ni muhimili mkubwa katika safu ya ulinzi ya Baroka, na amekuwa msaada mkubwa hasa pale timu inapotafuta matokeo.  Katika msimu wake wa kwanza 2017/ 2018 ameifungia klabu yake magoli 3 katika mechi 28 alizocheza na kuisaidia timu hiyo kumaliza katika nafasi ya 14 katika ligi kuu ya Afrika Kusini inayojulikana kwa jina la ABSA. Mwishoni mwa mwaka huu, Banda aliisadia Baroka Fc kubeba kombe kubwa zaidi katika historia yao kama klabu linalojulikana kama  telcom Knockout. Mwaka huu pekee katika msimu wa 2018/2019 amecheza mechi  11 kati ya 15  ametumia  dakika 961 kuitumikia klabu hiyo  kama beki wa kati tegemeo na kuisaidia Baroka kukusanya alama 14, wakishinda mechi 3, sare 5 na kupoteza 7 na kuwaweka katika nafasi ya 12 kati ya timu 16 zilizopo. Abdi Banda amekuwa akiitwa katika kila mahindano yanayoihusisha timu ya taifa , taifa Stars. Hadi sasa amecheza  mechi 5 za Taifa Stars, 2 zikiwa ni za kirafiki na 3 za kufuzu AFCON kwa ujumla ametumia dakika 412 kulitumikia taifa lake kwa mwaka huu pekee.

Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji)- Mwaka 1992 ndiyo mwaka ambao ulimleta Mbwana Ally Samatta, mfungaji bora wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Africa Mwaka 2015. Mwaka ambao alifunga magoli 7 na kuiwezesha timu yake ya TP Mazembe kuchukua ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Africa mwaka 2015. Mwaka 2016 alikuwa mchezaji bora wa Africa kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya Africa.

Ndiye mshambuliaji wa Genk ambaye amefunga magoli 31 mpaka sasa kwenye mechi 73. Huku timu ya Taifa akiwa amefunga magoli 17 katika mechi 45. Msimu huu amefunga magoli 14 kwenye ligi kuu ya Ubelgiji.

Simon Msuva ( DHL d’el-Jadida, Morocco)Aliwahi kufanya vizuri akiwa na jezi ya njano na kijani katika mitaa ya jangwani. Kitu ambacho kilimpa nafasi yeye ya kupata nafasi ya kucheza soka la kulipwa katika ligi kuu ya Morroco. Mwaka 2018 ulikuwa msimu wake wa kwanza akicheza soka la kulipwa na alifanikiwa kufunga magoli 11. Mafanikio ambayo ni makubwa ukilinganisha ni Mara ya kwanza kwake yeye kucheza kwenye klabu ambayo ilikuwa na utamaduni tofauti na klabu aliyotoka.


Timu ya Mwaka

  • Azam Fc (0%, 0 Votes)
  • Lipuli Fc (0%, 0 Votes)
  • Simba Sc (0%, 0 Votes)
  • Yanga Sc (0%, 0 Votes)

Jumla ya Kura: 0

Loading ... Loading ...

Kocha yupi ni Bora zaidi?

Hans Van Pluijm (Singida Utd, Azam Fc)- Alikuwa na mafanikio kiasi wakati akiwa na Singida Utd msimu uliopita. Juni mwaka huu aliifikisha Singida United fainali ya kombe la FA ambayo walipoteza 3-2 mbele ya Mtibwa Sugar FC. Hans aliisaidia Singida kumaliza nafasi ya tano katika ligi kuu Mei mwaka huu. Alipojiunga na Azam FC hakuchukua muda mrefu akawapa taji la Cecafa Kagame Cup Julai mwaka huu.
Licha ya Azam FC kuzidiwa alama kumi na viongozi wa ligi kuu Yanga SC, Hans amepoteza mchezo mmoja tu kati ya 18 aliyoisimamia.

Oscar Mirambo (U17)Kocha wa timu ya vijana ya Serengeti boys. Mwaka 2018 ulikuwa na mafanikio makubwa kwake, ambapo aliiwezesha Serengeti boys kushika nafasi ya tatu katika michuano maalumu ya kufuzu Afcon ya vijana waliochini ya umri wa miaka 17. Aliiwezesha pia kushinda kombe la COSAFA lililoshirikisha timu zilizochini ya umri wa miaka 17 kwa nchi za kusini mwa Africa , Tanzania ikiwa ni timu mwalikwa.

Zuberi Katwila (Mtibwa FC)- Ameipa Mtibwa kombe la Azam Sports Federation Cup  kwa kuifunga Singida Utd Katika fainali na kuiwezesha mtibwa  kushiriki mashindano ya shirikisho la Afrika (Caf) ikiwa ni mara ya 5 tangu  mwaka 2004. Mtibwa iliishia katika  raundi ya kwanza ya mashindano ya Shirikisho.Ameisaidia Mtibwa kumaliza katika nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi msimu wa 2017/18. Katika msimu huu, Mtibwa ipo katika nafasi ya 4 ikiwa na alama 26 ikicheza michezo  15 ikiwa ni tofauti ya  mechi 3 na anayeongoza ligi , Yanga SC akiwa na alama 50.Katwila  anasifika hasa zaidi katika mbinu za kimchezo pindi anakabiliana na timu kubwa, ndio maana  wengi hawashangai kuiona Mtibwa ikiifunga timu kama Azam, Yanga na Simba.


Unaguswa na uandishi wetu?

Loading ... Loading ...

Ni nani Kipa Bora zaidi?

Aishi Manula (Simba Sc)Amekua mchezaji muhimu katika mbio za ubingwa lakini pia kuipeleka simba katika hatua ya makundi ya klabu bingwa Africa!
Licha ya makosa yake ya kuruhusu kufungwa mabao ya mbali bado anabaki moja ya makipa imara kwa Simba na Taifa stars

Ramadhani Kabwili (Yanga SC)- Miongoni mwa wachezaji wadogo wenye msaada mkubwa kwa klabu zao na taifa kwa ujumla akitokea timu ya U20 ya Yanga . Kabwili mwenye miaka 18 amecheza mechi 4 akiwa na klabu yake ya Yanga katika michuano ya Shirikisho barani Afrika mwaka huu, akishinda 1, sare 1 na kufungwa mechi 2. Lakini pindi awapo langoni amekuwa akionyesha uhai kama kijana anayeweza kufanya makubwa zaidi ya yanayoonekana wakati wa mechi za Ligi Kuu pia.
Kwa upande wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Kabwili ameidakia mara 3, sare 1, dhidi ya Malawi 1-1,kufungwa mechi 1 dhidi ya Algeria 4-1 na kushinda moja dhidi ya Congo 2-0.

Razack Abalora (Azam Fc)- Huu ni msimu wake wa pili katika soka la Tanzania. Azam FC, Abarola ameonyesha kiwango cha juu kwa mwaka wote 2018. Hujipanga vizuri langoni, huongoza safu yake ya ulinzi, muhamasishaji, ni golikipa mzuri katika uchezaji wa mipira ya krosi na kona. Pia, amekuwemo kwenye kikosi kilicho chukua CECAFA mwaka 2018, na timu yake kushiriki vizuri Ligi Kuu. Ana sifa nyingi kama mchezaji wa kulipwa.


Nani anakufa?

  • Yanga Sc (0%, 0 Votes)
  • Simba Sc (0%, 0 Votes)
  • Sare (0%, 0 Votes)

Jumla ya Kura: 0

Loading ... Loading ...

Upi ni Usajili Bora?

Cletus Chota Chama (Simba Sc)-Mwamba wa Lusaka, mchezaji mwenye miguu mitamu inayopika mpira mtamu. Inawezekana sura yake isikuvutie kumtazama lakini miguu yake inavutia kutazamwa, ina kila aina ya urembo, urembo ambao umesababisha mpaka sasa hivi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Africa kuhusika katika magoli manane kwenye mechi nne. Akiwa amefunga magoli manne na kutoa pasi nne za mwisho za magoli. Na kwenye ligi kuu ya Tanzania bara akiwa ametoa pasi nne za mwisho

Feisal Salum (Yanga ScMchezaji wa Yanga SC, katika nafasi ya kiungo cha kati. Ana umri wa miaka 20. Alisajiliwa na Yanga Augosti 15, 2018 akitokea JKU ya Zanzibar.
Ameitumikia Yanga katika mechi 2 za mwisho za makundi za Mashindano ya Shirikisho Afrika na takribani mechi zote za ligi kuu Tanzania Bara (TPL)
Tangu asajiliwe ameitumikia Yanga katika nafasi ya kiungo cha kati kwa uhai mkubwa. Ameituliza timu, akisaidiana na Papy Tshishimbi kuipandisha timu na kuongeza presha kwa timu pinzani.
Anasifika kwa kupiga pasi sahihi kwa mtu sahihi na kwa wakati sahihi. Anafunga pale panapohitajika kufanya hivyo kwa kuibeba timu.
Ameisaidia timu yake kumaliza mwaka 2018 ikiwa katika nafasi ya kwanza , ikijikusanyia alama 50. Fei Toto ni chaguo la kwanza la kocha Mwinyi Zahera katika kikosi cha Yanga

Nicholas Wadada (Azam FC) – Beki wa pembeni wa Mabingwa mara moja wa Tanzania Bara Azam FC na timu ya Taifa ya Uganda, ana umri wa miaka 24 tu na huu ukiwa na msimu wake wa kwanza kwenye ligi kuu soka Tanzania Bara tangu alipotua nchini akitokea Vipers ya Uganda, ametumika karibu kila mchezo ambao Azam imecheza mpaka sasa kwenye ligi akiisaidia kushika nafasi ya pili wakia na alama 40 mpaka sasa. Akisaidiana na mabeki wengine ameiwezesha Azam kuwa miongoni mwa timu zenye ngome kali ambapo mpaka sasa imeruhusu nyavu zake kuguswa mara nane pekee.

Meddie Kagere (Simba sc)  Mshambuliaji wa Simba SC na timu ya taifa ya Rwanda, alijiunga na Simba akitokea klabu ya Gor Mahia FC ya Kenya Julai Mosi Mwaka huu.
Mwanzoni tu mwa usajili wake aliisaidia Simba kufika fainali za kombe la Kagame, aliisaidia Simba kushinda ngao ya jamii dhidi ya Mtibwa Sugar, Kagere alifunga goli la kwanza katika ushindi wa goli 2-1.
Ameshawahi kupata tuzo ya mchezaji bora wa mwezi agosti mwaka huu katika ligi ya TPL.
Ameisaidia Simba katika michezo mbalimbali ikiwemo ya ligi na hata kimataifa. Ana goli 3 katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika , ana magoli 7 ligi kuu Tanzania Bara.
Amekuwa ni muhimili mkubwa kwa timu yake ya Simba na timu ya Taifa. Kagere anajinasibisha kwa uwezo wake kufunga magoli, kutumia nguvu na kasi wakati akilitazama lango la mpinzani.


Sorry, there are no polls available at the moment.

Nani Chipukizi Bora?

Habibu Kiyombo (Singida Utd)Mwaka 2018 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwake. Ulikuwa mwaka ambao alijiyambulisha rasmi kwenye soko la biashara la mpira. Aliiwezesha Mbao Fc ibaki ligi kuu Tanzania bara kwa miguu yake bora. Miguu ambayo ilimpa nafasi ya kusajiliwa na Singida United, sehemu ambayo ilimpa nafasi ya kwenda kufanya majaribio Afrika Kusini kwenye timu ya Mamelodi Sundowns

Kelvin John (U23) -Jiji la mwanza ndiyo lilitoa Mwamba uliotengeneza jina la Kelvin John. Kipaji ambacho kilifananishwa na Mbappe. Mwaka huu akiwa na Serengeti boys alifanikiwa kuwa mfungaji bora wa michuano ya kufuzu Afcon mwaka 2019. Mwaka huu pia alifanikiwa kuiongoza Serengeti boys katika michuano ya vijana iliyofanyika Angola na Serengeti boys kuchukua ubingwa. Amefanikiwa kufanya majaribio nchini Ubelgiji na nchini Afrika Kusini katika klabu ya Ajax Town

Ramadhani Kabwili (Yanga Sc)-Miongoni mwa wachezaji wadogo wenye msaada mkubwa kwa klabu zao na taifa kwa ujumla akitokea timu ya U20 ya Yanga . Kabwili mwenye miaka 18 amecheza mechi 4 akiwa na klabu yake ya Yanga katika michuano ya Shirikisho barani Afrika mwaka huu, akishinda 1, sare 1 na kufungwa mechi 2. Lakini pindi awapo langoni amekuwa akionyesha uhai kama kijana anayeweza kufanya makubwa zaidi ya yanayoonekana wakati wa mechi za Ligi Kuu pia.
Kwa upande wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Kabwili ameidakia mara 3, sare 1, dhidi ya Malawi 1-1,kufungwa mechi 1 dhidi ya Algeria 4-1 na kushinda moja dhidi ya Congo 2-0.


How do i rate my player?

  • Mayele (29%, 10 Votes)
  • Bangala (17%, 6 Votes)
  • Farid (14%, 5 Votes)
  • Feisal (11%, 4 Votes)
  • Kibwana (9%, 3 Votes)
  • Lomalisa (9%, 3 Votes)
  • Aziz ki (9%, 3 Votes)
  • Job (3%, 1 Votes)
  • Sure boy (0%, 0 Votes)
  • Diarra (0%, 0 Votes)
  • Moloko (0%, 0 Votes)

Jumla ya Kura: 16

Loading ... Loading ...

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x