Video

Napata burudani kumwangalia Marcel Bonaventure lakini sijui mwakani itakuaje!

Sambaza....

Marcel Boniventure Kaheza “Rivaldo”  jezi namba 10 ya Majimaji huku pia akicheza nafasi hiyohiyo kama ya jezi yake namba 10 uwanjani.

Kwa sasa ndie mchezaji tegemeo pale kwa wakazi wa Songea katika timu ya Majimaji. Huku wakiwa wanapambana timu isishuke daraja kwa kiasi kikubwa Marcel ndie anaeongoza kwenye uwanja wa vita ili kuinusuru Majimaji isishuke daraja.

Mechi zilizobaki za Majimaji FC

Mpaka sasa ana magoli 10 katika Ligi Kuu Bara (VPL) huku kinara akiwa ni Emmanuel Okwi wa SimbaSc. Huku timu yake ya Majimaji ikiwa nafasi ya pili kutoka mkiani ( ya 15).

Kwa nafasi ya timu yake ilipo na nafasi ya Marcel Boniventure katika chati ya ufungaji bora unaweza kuona ni vitu viwili tofauti, na kunifanya niamini ni juhudi binafsi ndizo zinazomfanya awepo pale.

Ni moja ya vipaji halisi vya soka ambavyo Tanzania inajivunia, ambapo kwa kiasi kikubwa kilichangiwa au kugunduliwa na klabu ya soka ya SimbaSc. Wakati klabu hiyo ilipokua na mifumo thabiti ya kukuza na kuedeleza vijana. Marcel ni zao lá Simba B, na hapa ndipo nchi inafaidi matunda ya  Simba katika uwekezaji wa vijana.

Kwa sasa ukiiangalia timu ya Majimaji inavyocheza ni wazi kabisa kwa kiasi kikubwa inamtegemea Marcel katika upatikanaji wa mabao yake. Iwe kwa kutoa msaada au kufunga yeye mwenyewe.

Ball brain, Ball balance na Ball technique “Triple B”. Zote Marcel zimetimia kwa Marcel na anazitumia kwa hali ya juu akiwa uwanjani.

Hatma Yake Ya Msimu Ujao

Ukiiangalia Majimaji ipo katika hali mbaya katika msimamo wa ligi ikiendelea kupambana isishuke.

Swali ni je kama Majimaji ikishuka mpaka Ligi Daraja La Kwaza atakushuka nayo au yeye atabaki?

Jibu ni rahisi tuu kwa mchezaji wa kariba ya Marcel Boniventure ni rahisi kwa timu kushuka daraja na yeye akabaki ligi Kuu. Kwa uwezo alionao naamini ni timu nyingi zitataka kumsaijili ili Kupata huduma yake.

Pia Majimaji ikifanikiwa kubaki Ligi Kuu sio rahisi kwake kuendelea kubaki Songea na kuendelea kuchezea timu inayopigania isishuke daraja karibia kila msimu. Huenda timu zetu kubwa zikaingia vitani ili kumsajili, kitu ambacho kitampunguzia mzigo wa kunusuru timu isishuke daraja na kugombea ubingwa.

Pia wakati anahojiwa na kituo fulani cha TV alisema kocha wake wa zamani wa Majimaji Kally Ongala alimtafutia timu ya kwenda kufanya majaribio nchini Sweden. Je ni kweli ataelekea huko kama alivyoeleza? Tusubiri tuone.

Lakini pia napata mashaka huenda akasajiliwa na hizi timu zetu kubwa na kushindwa kupata nafasi ya kucheza kila weekend kutokana na mifumo ya timu zetu kama ambavyo tunashindwa kuwafaidi hivi sasa kina Mwambeleko, Raphael Daud,  Ally Shomary.

Hivyo basi ni vyema akaenda timu itakayompa nafasi ya kucheza kila mwisho wa wiki ili kuendelea kufurahia kipaji chake na sisi mashabiki kuendelea kupata burudani ya kipaji chake na kuendelea kumuona kila mwisho wa wiki.

Nina subiri kwa hamu kuiona mwakani ya Marcel Boniventure Kaheza katika maisha yake ya soka.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x